SIMULIZI: “JENEZA LA AJABU ” **SEHEMU YA 03* - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Hadithi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=48) +---- Thread: SIMULIZI: “JENEZA LA AJABU ” **SEHEMU YA 03* (/showthread.php?tid=960) |
SIMULIZI: “JENEZA LA AJABU ” **SEHEMU YA 03* - MwlMaeda - 08-20-2021 SIMULIZI: “JENEZA LA AJABU “ **SEHEMU YA 03*
Msitu wa Majini;
Ilikua mida ya jioni siku ya jumatatu ,
tetemeko la kutisha linatokea katika msitu wa majini,Malikia wa msituni, kiongozi aliyemiliki msitu na kuongoza viumbe vyote vilivyopatikana ndani ya msitu anaamua kuitisha kikao, kwani tetemeko lile liliashiria jambo fulani, kama ilivyozoeleka katika msitu huo, tetemeko likitokea basi muda wowote msitu ulikua hatarini kuvamiwa. “Ndugu zangu
majini, mapepo na mizimu ya mababu zetu, msitu wetu uko hatarini kuvamiwa ,na niwajibu wetu kuulinda msitu huu, pia inatakiwa tulipize kisasi kwani mtu anayekuja kuvamia msitu huu, baba yake aliwahi kuja hapa msituni na kuua ndugu zetu na kisha kutokomea na baadhi ya mali zetu ili awe mganga na mtabili hodari, japo ameshapoteza maisha “,malikia alizungumza kwa hasira, katika kikao cha ghafla alichokiitisha muda mfupi baada ya tetemeko kutokea, huku umati wa viumbe hatari sana wa msitu wa majini, msitu uliokua na utajiri mwingi, zikiwemo dhahabu na almasi, wakiwa makini kumsikiliza malikia wao na kujiandaa na mapambano. “Aiweeee mtukufu
malikia wa msitu huu,tuko tayali kutekeleza maagizo yako, na kuua chochote kitakachokanyaga ardhi hii “,ilikua ni sauti ya majini waliohudhuria kikao, huku wakijawa na uchu wa kulipiza kisasi hasa wakikumbuka jinsi mzee Nyangoma, baba yake Njoshi jinsi alivyofanikiwa kuiba mkanda pamoja na panga lenye nguvu za ajabu, na kutoroka navyo huku akiua baadhi ya majini, kitendo kilichowakasilisha viumbe wote wa msituni. Ikulu kwa mfalme;
Kijana Njoshi anafika ikulu kwa mfalme
na kushangazwa na jambo aliloliona mbele ya macho yake, hali ya mfalme ilikua mbaya sana kiasi kwamba hakuweza hata kuinuka kitandani wala kufungua kinywa chake na kutamka neno lolote lile, kwa upande mwingine alitamani mfalme apoteze maisha kwani aliona ndio utakuwa mwanzo wa ardhi ya Mwamutapa kuwa huru kutoka katika uongozi wake wa kidikteta ,na pia yatakua ndio malipo ya dhambi zote za mauaji aliyoyafanya, huku baba yake akiwa miongoni mwa watu waliouawa kikatili na mfalme. Njoshi akiwa bado
amepigwa na butwaa, alianza kupata picha kuwa inawezekana aliweza kudanganywa kuwa aliitwa na mfalme ili aozeshwe Grace,kwani kwa wakati ule, machozi ya huzuni hayakukatika machoni kwa Grace,na kumfanya aamini mawazo yake, kuwa palikuwa na tatizo nyumbani kwa mfalme. “Aiweeeeeh mtukufu
mfalme, mtumwa wako Njoshi Nyangoma nimeitika wito wako, aiweeeeh ……mfalme Mutapa udumu milele”,Njoshi aliongea huku akiwa amesimama mbele ya kitanda cha mfalme, huku familia nzima ikiwa imekaa kimya, wakimuomba Mungu Njoshi akubaliane na ombi la mfalme, kwani waliamini mfalme hata akipoteza maisha ataweza kufufuka ndani ya wiki moja, jambo ambalo lingewezekana kama angezikwa ndani ya jeneza la ajabu, jeneza ambalo Njoshi inatakiwa akalitengeneze kwa kutumia miti inayopatikana katikati ya msitu wa majini na kisha kuja nalo ikulu kwa mfalme. “Kijana wangu
“Ndiyo mfalmeNjoshi, utafanikiwa kumuoa binti yangu Grace, na kumiliki nusu ya ufalme wangu, kama tu ukikubali kwenda katika msitu wa majini, na kutengeneza jeneza kisha kuja nalo hapa “,yalikuwa ni maneno yaliyoandikwa kwa maandishi na mfalme, maneno ambayo Njoshi aliyasoma na kisha hofu ya kifo kumuandama, kwani hakuna mtu aliyewahi kupona kutoka katika msitu wa majini, isipokuwa baba yake pekee.Njoshi alikumbuka maneno ya mama yake alimwambia kuhusu hatari hii, na kisha kumsihi asikatae kwenda kwani huko msituni ndiyo sehemu pekee ya kuupata ufalme, pia Njoshi alikumbuka siraha alizopewa na mama yake na kuziweka ndani ya begi kisha kumsihi asiweze kulitupa begi hilo. wangu mtukufu, nimekubali, aiweeeh mfalme udumu milele, “Njoshi alikubali ombi la mfalme, na kufanya nyuso za familia nzima ya mfalme kutabasamu kwa furaha, isipokuwa Grace, kwani hakutaka mpenzi wake kwenda msituni ndio maana alikuwa akilia toka mwanzoni, na wala hakulizwa na hali mbaya ya baba yake aliyonayo, bali jambo ambalo Njoshi aliweza kuitiwa ikulu, lilikuwa la hatari sana na aliamini atampoteza mpenzi wake kama atakubali ombi la baba yake. |