MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
SIMULIZI: “JENEZA LA AJABU ” *SEHEMU YA 5*

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
SIMULIZI: “JENEZA LA AJABU ” *SEHEMU YA 5*
#1
SIMULIZI: “JENEZA
LA AJABU “
*SEHEMU YA 5*
Giza likiwa linazidi
kuwa la kutisha,ikiwa imefika mida kama ya saa nne usiku, kijana Njoshi akiwa
amevalia bukta yake nyeusi, huku chini akiwa miguu peku, kwani watu wa
Mwanamutapa kutokuvaa viatu ilikuwa kama tamaduni yao, kijana Njoshi aliendelea
kutembea huku akinyosha balabala kubwa ya vumbi, balabala iliyokuwa
ikiunganisha nchi ya Mwamutapa na nchi zingine za jirani, ikiwemo nchi ya
Mwamuyeshi. Sauti za miguu yake ndizo zilizosikika balabala nzima, kwani watu
hawakupita balabala hiyo mida ya usiku, kutokana na kuogopa kutekwa na
kunyanganywa mali zao, na pengine hata kuuawa.
Ilikuwa tofauti kwa
Njoshi, hakuogopa jambo lolote lile, akiwa kifua mbele kwani hakuvaa shati
lolote lile huku akiwa amebeba begi jeusi alilopewa na mama yake, aliendelea
kusonga mbele huku akitembea kwa mwendo wa haraka, na muda mwingine alikimbia,
ili aweze kufika katika ardhi ya msitu wa majini kabla hapajakucha siku ya
jumanne.
“Mpaka sasa
nimeshakimbia umbali mrefu sana, sina budi kuongeza bidii “,Njoshi
aliongea peke yake moyoni mwake, huku akiwa tayali ameshayaacha majumba ya
Mwanamutapa mbali sana. Kila alipokumbuka mateso yote ya Wanamutapa, nguvu za
ajabu ziliongezeka mwilini mwake na kumfanya azidi kuongeza mwendo ili apate
kuikomboa nchi yake haraka sana, huku mbalamwezi ikiangaza vema njia
aliyotakiwa kupita. “Hahaha eti jeneza, siamini kama kuna watu hawataki
kufa, yani uishi milele, na kututesa milele, hili ni jambo ambalo haliwezekani
“,Njoshi aliongea maneno ya kejeli kwa mfalme, huku akitabasamu na kumuona
mfalme kama mtu wa ajabu sana, mtu aliyemkabidhi fisi bucha na kula nyama zote
za buchani.
“Hapa mimi
ninachofuata ni fimbo ya ufalme, fimbo ambayo inapatikana katika ngome ya
malikia wa msituni, malikia wa majini, jeneza nitalishughulikia nikishapata
fimbo yangu ya kuiongoza Mwanamutapa “,Njoshi alizidi kuongea peke yake,
huku akisisitiza jambo lililompeleka msituni, kwani ili uwe mfalme nilazima
umiliki fimbo ya kifalme kutoka katika msitu huo, na mfalme Mutapa aliipata
fimbo hiyo ya uongozi kutokana na kurithi kwa wazazi wake,huku chanzo cha fimbo
hiyo kikisemekana ni katika msitu wa majin. Fimbo hiyo ilimpatia mamlaka mfalme
kutodhurika na majini wa msituni, kwani msitu wa majini ulipatikana katika nchi
ya Mwamutapa. Wengi walifunga safari kwenda msituni kuchukua fimbo nyingine ya
ufalme, inayofanana na fimbo ya mfalme lakini walishindwa kurudi wakiwa hai.
Pia wasingeweza
kupambana na mfalme kwani fimbo aliyonayo ilimpatia kiburi sana, hata
ukilishinda jeshi lake na kumuua, usingeweza kuongoza nchi, kwani fimbo
iliandikwa jina  la mfalme Mutapa,. Hivyo
njia ambayo ni rahisi, ilikuwa ni kuitafuta fimbo ya ufalme msituni ,na
kuiandika jina lako binafsi ili majini wakutambue na wasikusumbue katika
uongozi wako,hapo ndipo ufanye mapinduzi na kumuua mfalme ili uongoze nchi ya
Mwanamutapa.
“Ngoja nipumzike
kidogo hapa chini ya mti ,ninywe maji, nichukue siraha zangu kwani muda wowote
nitaufikia msitu “,Njoshi aliongea huku akiketi katika majani mafupi chini
ya mti wa ubuyu, na kisha kufungua begi alilopewa na mama yake. Huzuni ya kutokumuona
tena mama yake ilimuandama, kwani aliyakumbuka maneno ya mama yake kuwa
hatomuona tena na kufanya machozi kumtoka , mithili ya mtu aliyefiwa na mtu
anayemtegemea. Alifungua begi na kutoa kitambaa cheusi, kitambaa ambacho
alitakiwa akifunge kiunoni kama mkanda, huku akishikilia panga kali, panga
ambalo linauwezo wa kuua majini. Ikiwa tayali imeshafika mida ya saa saba
usiku, Njoshi ananyanyuka sehemu aliyokuwa amepumzika kwa takribani dakika
tano, na kisha kusonga mbele kuusogelea msitu wa majini.
Msitu wa majini
Malikia wa majini anaingiliwa na hofu
kubwa sana kwani mtu aliyekuwa anakuja kuuvamia msitu alionekana kuwa hatari
sana, kwani kila alipojaribu kumtambua sura yake alishindwa, na ghafla
mawasiliano yalipotea, hakuweza kumuona tena katika kiganja chake, kiganja
kilichokuwa kikimuonesha mtu aliyekuwa njiani akielekea msituni. “Huyu
anayekuja huku natambua kuwa ni mtoto wa mtu aliyewahi kuja huku na kutuibia
mali zetu, lakini sura yake ningependa niifahamu lakini nimeshindwa, na kwanini
kapotea ghafla, nashindwa kumuona tena katika viganja vyangu “,Malikia wa
msituni alizungumza kwa hasira na mshangao mkubwa, bila kutambua kuwa Njoshi
aliweza kuvaa kitambaa cheusi kiunoni, na kumfanya kutoonekana kama akiwa
anafuatiliwa na majini.
“Hapa nikizubaa,
watu wangu watakufa “,malikia  wa
majini, msichana aliyekuwa mrembo sana, na mwenye umri sawa na Grace,
alizungumza huku akitafuta kichupa kidogo cha maji, na kisha kumpatia askari
wake mmoja, kunyunyizia maji hayo kuzunguka ngome yake yote ili kujilinda. Maji
hayo yalikuwa na uwezo wa kumgandisha mahali pale, mtu yeyote mwenye asili ya
ubinadamu, atakapokanyaga eneo lile.
“Hapa tayali
nimemaliza kazi, hata kama akifanikiwa kuwapita askari wangu msituni, mimi
lazima nitamkamata “,malikia aliongea kwa kujigamba, na kuachia tabasamu
zuri lililoonesha vema uzuri wake.
Nje ya msitu;
        Kwa mbali kijana shupavu na hodari
Njoshi Nyangoma, anakamatilia panga lake kisawasawa, kwani alianza kuuona msitu
hatari wa majini, ukiwa kama hatua mia moja mbele yake, baada ya kutembea na
kukimbia kwa usiku mzima, na ilikua imeshafika mida ya saa kumi usiku, kuamkia
siku ya jumanne.
“Aiweeeh mizimu wa
mababu zangu, mizimu wa ardhi ya Mwamutapa, asanteni kwa kunifikisha salama,
naomba mnilinde tena na kunirudisha nyumbani salama “,Njoshi aliongea kwa
hofu na woga, kwani alikuwa na kazi nzito, tena ya hatari ikiwa mbele yake.
“Hapa ni mwendo wa
kuua tu kiumbe chochote, kitakachokatiza mbe…le…y…a…ngu “,Njoshi
alishindwa kumalizia sentesi yake baada ya kukanyaga mtego wa kamba, na kisha
mtego huo kumning’iniza juu ya mti huku miguu ikiwa juu na kichwa kikiwa chini,
mala tu alipokanyaga mguu wake msituni.
Njoshi bila kupoteza
muda, aliikata kamba ile mguuni kwake, kwa kutumia panga lake na kisha kudondoka
chini kama mzigo huku akiwa haamini kilichokuwa kimetokea ghafla namna ile, na
kumuongezea hofu na woga huku akitakiwa kuwa makini sana ndani ya msitu.
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)