SIMULIZI: “JENEZA LA AJABU ” *SEHEMU YA 5* - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Hadithi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=48) +---- Thread: SIMULIZI: “JENEZA LA AJABU ” *SEHEMU YA 5* (/showthread.php?tid=958) |
SIMULIZI: “JENEZA LA AJABU ” *SEHEMU YA 5* - MwlMaeda - 08-20-2021 SIMULIZI: “JENEZA LA AJABU “ *SEHEMU YA 5*
Giza likiwa linazidi
kuwa la kutisha,ikiwa imefika mida kama ya saa nne usiku, kijana Njoshi akiwa amevalia bukta yake nyeusi, huku chini akiwa miguu peku, kwani watu wa Mwanamutapa kutokuvaa viatu ilikuwa kama tamaduni yao, kijana Njoshi aliendelea kutembea huku akinyosha balabala kubwa ya vumbi, balabala iliyokuwa ikiunganisha nchi ya Mwamutapa na nchi zingine za jirani, ikiwemo nchi ya Mwamuyeshi. Sauti za miguu yake ndizo zilizosikika balabala nzima, kwani watu hawakupita balabala hiyo mida ya usiku, kutokana na kuogopa kutekwa na kunyanganywa mali zao, na pengine hata kuuawa. Ilikuwa tofauti kwa
Njoshi, hakuogopa jambo lolote lile, akiwa kifua mbele kwani hakuvaa shati lolote lile huku akiwa amebeba begi jeusi alilopewa na mama yake, aliendelea kusonga mbele huku akitembea kwa mwendo wa haraka, na muda mwingine alikimbia, ili aweze kufika katika ardhi ya msitu wa majini kabla hapajakucha siku ya jumanne. “Mpaka sasa
nimeshakimbia umbali mrefu sana, sina budi kuongeza bidii “,Njoshi aliongea peke yake moyoni mwake, huku akiwa tayali ameshayaacha majumba ya Mwanamutapa mbali sana. Kila alipokumbuka mateso yote ya Wanamutapa, nguvu za ajabu ziliongezeka mwilini mwake na kumfanya azidi kuongeza mwendo ili apate kuikomboa nchi yake haraka sana, huku mbalamwezi ikiangaza vema njia aliyotakiwa kupita. “Hahaha eti jeneza, siamini kama kuna watu hawataki kufa, yani uishi milele, na kututesa milele, hili ni jambo ambalo haliwezekani “,Njoshi aliongea maneno ya kejeli kwa mfalme, huku akitabasamu na kumuona mfalme kama mtu wa ajabu sana, mtu aliyemkabidhi fisi bucha na kula nyama zote za buchani. “Hapa mimi
ninachofuata ni fimbo ya ufalme, fimbo ambayo inapatikana katika ngome ya malikia wa msituni, malikia wa majini, jeneza nitalishughulikia nikishapata fimbo yangu ya kuiongoza Mwanamutapa “,Njoshi alizidi kuongea peke yake, huku akisisitiza jambo lililompeleka msituni, kwani ili uwe mfalme nilazima umiliki fimbo ya kifalme kutoka katika msitu huo, na mfalme Mutapa aliipata fimbo hiyo ya uongozi kutokana na kurithi kwa wazazi wake,huku chanzo cha fimbo hiyo kikisemekana ni katika msitu wa majin. Fimbo hiyo ilimpatia mamlaka mfalme kutodhurika na majini wa msituni, kwani msitu wa majini ulipatikana katika nchi ya Mwamutapa. Wengi walifunga safari kwenda msituni kuchukua fimbo nyingine ya ufalme, inayofanana na fimbo ya mfalme lakini walishindwa kurudi wakiwa hai. Pia wasingeweza
kupambana na mfalme kwani fimbo aliyonayo ilimpatia kiburi sana, hata ukilishinda jeshi lake na kumuua, usingeweza kuongoza nchi, kwani fimbo iliandikwa jina la mfalme Mutapa,. Hivyo njia ambayo ni rahisi, ilikuwa ni kuitafuta fimbo ya ufalme msituni ,na kuiandika jina lako binafsi ili majini wakutambue na wasikusumbue katika uongozi wako,hapo ndipo ufanye mapinduzi na kumuua mfalme ili uongoze nchi ya Mwanamutapa. “Ngoja nipumzike
kidogo hapa chini ya mti ,ninywe maji, nichukue siraha zangu kwani muda wowote nitaufikia msitu “,Njoshi aliongea huku akiketi katika majani mafupi chini ya mti wa ubuyu, na kisha kufungua begi alilopewa na mama yake. Huzuni ya kutokumuona tena mama yake ilimuandama, kwani aliyakumbuka maneno ya mama yake kuwa hatomuona tena na kufanya machozi kumtoka , mithili ya mtu aliyefiwa na mtu anayemtegemea. Alifungua begi na kutoa kitambaa cheusi, kitambaa ambacho alitakiwa akifunge kiunoni kama mkanda, huku akishikilia panga kali, panga ambalo linauwezo wa kuua majini. Ikiwa tayali imeshafika mida ya saa saba usiku, Njoshi ananyanyuka sehemu aliyokuwa amepumzika kwa takribani dakika tano, na kisha kusonga mbele kuusogelea msitu wa majini. Msitu wa majini
Malikia wa majini anaingiliwa na hofu
kubwa sana kwani mtu aliyekuwa anakuja kuuvamia msitu alionekana kuwa hatari sana, kwani kila alipojaribu kumtambua sura yake alishindwa, na ghafla mawasiliano yalipotea, hakuweza kumuona tena katika kiganja chake, kiganja kilichokuwa kikimuonesha mtu aliyekuwa njiani akielekea msituni. “Huyu anayekuja huku natambua kuwa ni mtoto wa mtu aliyewahi kuja huku na kutuibia mali zetu, lakini sura yake ningependa niifahamu lakini nimeshindwa, na kwanini kapotea ghafla, nashindwa kumuona tena katika viganja vyangu “,Malikia wa msituni alizungumza kwa hasira na mshangao mkubwa, bila kutambua kuwa Njoshi aliweza kuvaa kitambaa cheusi kiunoni, na kumfanya kutoonekana kama akiwa anafuatiliwa na majini. “Hapa nikizubaa,
watu wangu watakufa “,malikia wa majini, msichana aliyekuwa mrembo sana, na mwenye umri sawa na Grace, alizungumza huku akitafuta kichupa kidogo cha maji, na kisha kumpatia askari wake mmoja, kunyunyizia maji hayo kuzunguka ngome yake yote ili kujilinda. Maji hayo yalikuwa na uwezo wa kumgandisha mahali pale, mtu yeyote mwenye asili ya ubinadamu, atakapokanyaga eneo lile. “Hapa tayali
nimemaliza kazi, hata kama akifanikiwa kuwapita askari wangu msituni, mimi lazima nitamkamata “,malikia aliongea kwa kujigamba, na kuachia tabasamu zuri lililoonesha vema uzuri wake. Nje ya msitu;
Kwa mbali kijana shupavu na hodari
Njoshi Nyangoma, anakamatilia panga lake kisawasawa, kwani alianza kuuona msitu hatari wa majini, ukiwa kama hatua mia moja mbele yake, baada ya kutembea na kukimbia kwa usiku mzima, na ilikua imeshafika mida ya saa kumi usiku, kuamkia siku ya jumanne. “Aiweeeh mizimu wa
mababu zangu, mizimu wa ardhi ya Mwamutapa, asanteni kwa kunifikisha salama, naomba mnilinde tena na kunirudisha nyumbani salama “,Njoshi aliongea kwa hofu na woga, kwani alikuwa na kazi nzito, tena ya hatari ikiwa mbele yake. “Hapa ni mwendo wa
Njoshi bila kupotezakuua tu kiumbe chochote, kitakachokatiza mbe…le…y…a…ngu “,Njoshi alishindwa kumalizia sentesi yake baada ya kukanyaga mtego wa kamba, na kisha mtego huo kumning’iniza juu ya mti huku miguu ikiwa juu na kichwa kikiwa chini, mala tu alipokanyaga mguu wake msituni. muda, aliikata kamba ile mguuni kwake, kwa kutumia panga lake na kisha kudondoka chini kama mzigo huku akiwa haamini kilichokuwa kimetokea ghafla namna ile, na kumuongezea hofu na woga huku akitakiwa kuwa makini sana ndani ya msitu. |