05-24-2022, 06:16 AM
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA MANENO ' RIZIKI' na 'ARZAKI'
Neno *riziki* katika lugha ya Kiswahili ni nomino [ *Ngeli: i-/zi-]* yenye maana zifuatazo:
1. Mahitaji ya msingi kama vile chakula anachopata mtu aghalabu baada ya kufanya kazi; malipo, ujira.
2. Baraka anazopata mtu katika maisha kutoka kwa Mwenyezi Mungu; neema.
Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *riziki* limetokana na neno la Kiarabu *rizqun* (soma: *rizqun/rizqan/rizqin رزق* ) lenye maana zifuatazo:
1. Kila kinachomnufaisha mtu kama vile chakula na mavazi.
2. Kinacholiwa kikafika tumboni; kilichoruzukiwa, marzuuq مرزوق maruzuku.
3. Mvua, sababu ya kupatikana chakula.
4. Ujira anaolipwa mtu kwa kazi aliyoifanya; mshahara.
3. Upole na huruma.
4. Moyo wa huruma.
5. Anachoruzukiwa mtu na Mwenyezi Mungu.
Kinachodhihiri ni kuwa neno hili ( *rizqun/rizqan/rizqin رزق*) lilipoingia katika lugha ya Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *riziki* maana yake katika Kiarabu haikubadilika.
Neno *arzaki* katika lugha ya Kiswahili ni nomino [ *Ngeli: i-/zi-]* iliyo wingi wa neno riziki.
Neno hili *arzaki* (soma: *arzaaqun/arzaaqan/arzaaqin ارزاق* ) katika lugha ya Kiarabu ni wingi wa neno 'rizqun' kama lilivyofafanuliwa hapo juu.
Kinachodhihiri ni kuwa neno hili *arzaaqun*(soma: *arzaaqun/arzaaqan/arzaaqin ارزاق*) lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *arzaki* maana yake katika lugha asili - Kiarabu haikubadilika.
*Shukran sana.*
*Khamis S.M. Mataka.*

Mwl Maeda