01-03-2022, 10:42 AM
SHAIRI : KUFA KUFAANA
———————–
Kweli kufa kufaana, nimeyaelewa haya,
nikayapata tokana, na msiba ulikuwa,
upo kwa Bwana Njuguna, tajiri huko Iwawa,
kafiwa na mtu wake, ikawa kufa kufaana.
______
Jamaa na marafiki, na wandugu walifika,
nyumbani hapakaliki, watu walimiminika,
wengi ja kundi la nyuki, sehemu zote kutoka,
msibani walikaa, kwa Njuguna pakajaa.
_____
Wapo walilia sawa, kwa ndimi zote kulia,
na macho wakavimbiwa, kwa kukesha wakilia,
pilau walipogawa, hapo ndo wakatulia,
walipotafuna yote, wak’endeleza kulia.
_____
Kumbe hao walikuwa, walala miferejini,
na njaa kwao ikiwa, ni wa daima mwandani,
hata hawakuelewa, huo msiba wa nani?
kweli kufa kufaana, sasa nimeshaelewa.
_____
Rwaka rwa Kagarama,
Mshairi Mnyarwanda.
———————–
Kweli kufa kufaana, nimeyaelewa haya,
nikayapata tokana, na msiba ulikuwa,
upo kwa Bwana Njuguna, tajiri huko Iwawa,
kafiwa na mtu wake, ikawa kufa kufaana.
______
Jamaa na marafiki, na wandugu walifika,
nyumbani hapakaliki, watu walimiminika,
wengi ja kundi la nyuki, sehemu zote kutoka,
msibani walikaa, kwa Njuguna pakajaa.
_____
Wapo walilia sawa, kwa ndimi zote kulia,
na macho wakavimbiwa, kwa kukesha wakilia,
pilau walipogawa, hapo ndo wakatulia,
walipotafuna yote, wak’endeleza kulia.
_____
Kumbe hao walikuwa, walala miferejini,
na njaa kwao ikiwa, ni wa daima mwandani,
hata hawakuelewa, huo msiba wa nani?
kweli kufa kufaana, sasa nimeshaelewa.
_____
Rwaka rwa Kagarama,
Mshairi Mnyarwanda.
Mwl Maeda