SHAIRI : KUFA KUFAANA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI : KUFA KUFAANA (/showthread.php?tid=1965) |
SHAIRI : KUFA KUFAANA - MwlMaeda - 01-03-2022 SHAIRI : KUFA KUFAANA ———————– Kweli kufa kufaana, nimeyaelewa haya, nikayapata tokana, na msiba ulikuwa, upo kwa Bwana Njuguna, tajiri huko Iwawa, kafiwa na mtu wake, ikawa kufa kufaana. ______ Jamaa na marafiki, na wandugu walifika, nyumbani hapakaliki, watu walimiminika, wengi ja kundi la nyuki, sehemu zote kutoka, msibani walikaa, kwa Njuguna pakajaa. _____ Wapo walilia sawa, kwa ndimi zote kulia, na macho wakavimbiwa, kwa kukesha wakilia, pilau walipogawa, hapo ndo wakatulia, walipotafuna yote, wak’endeleza kulia. _____ Kumbe hao walikuwa, walala miferejini, na njaa kwao ikiwa, ni wa daima mwandani, hata hawakuelewa, huo msiba wa nani? kweli kufa kufaana, sasa nimeshaelewa. _____ Rwaka rwa Kagarama, Mshairi Mnyarwanda. |