hadhira huwa tuli hasa ikihifadhiwa kwa maandishi
(06-14-2021, 07:02 PM)MwlMaeda Wrote: MAJIBU:
- Kutoweka kwa mawasiliano ya ana kwa ana baina ya fanani na hadhira.
- Vitendo vya fanani na hadhira havionekani (kufifia kwa uhai na uhalisia wa fasihi simulizi)
- Kupungua kwa hadhi, ubora, ladha na mvuto wa kazi ya fasihi simulizi.
- Hupunguza na kubagua hadhira kutokana na njia za uhifadhi na uwasilishaji.
- uwasilishaji wake huwa wa muda mrefu kutokana na maandalizi yake.
- Kupunguza uwezo wa fanani kuhifadhi kazi za fasihi simulizi kichwani.
- Huzuia mabadiliko ya papo hapo
- Huingiza gharama kutokana na gharama za uandaaji na uhifadhi
- Huwa mali ya mtunzi badala ya jamii nzima