MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

Msamiati wa Kazi mbalimbali

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
Msamiati wa Kazi mbalimbali
#1
Katika dunia ya leo watu hufanya kazi mbalimbali ili waweze kushinda maisha ambayo tunaona ni magumu na ni lazima tupambane nayo kwa kufanya kazi mbalimbali ili tupate mkate wa leo na kesho. Huu ni msamiati wa watu wanaofanya kazi mbalimbali :

1. Dobi : Hufanya kazi ya kuosha nguo 
2. Karani : Anayeangalia matumizi ya pesa katika benki au kampuni fulani 
3. Katibu : Anayeweka rekodi za mambo na orodha mbalimbali katika kampuni au idara fulani 
4. Kungwi : Hufunza vijana jandoni 
5. Mchuuzi : Anayeuza bidhaa kutoka nyumba hadi nyumba 
6. Mfinyanzi : Hufinyanga udongo kutengeza vyombo kama vyungu, n.k 

7. Mhandisi : Anayefanya kazi ya kuunda au kurekebisha injini/mashine mbalimbali 
8. Mhasibu : Mtu anayefanya kazi ya hesabu 
9. Muhunzi : Hufua vyuma 
10. Mkutubi : Anayeweka rekodi za vitabu katika maktaba, na kuwasaidia wanaotaka kuomba vitabu. 
11. Tabibu : Anayetibu watu, daktari 
12. Topasi : Kazi ya kuosha vyoo.
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)