Msamiati wa Kazi mbalimbali - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=9) +--- Thread: Msamiati wa Kazi mbalimbali (/showthread.php?tid=1432) |
Msamiati wa Kazi mbalimbali - MwlMaeda - 11-10-2021 Katika dunia ya leo watu hufanya kazi mbalimbali ili waweze kushinda maisha ambayo tunaona ni magumu na ni lazima tupambane nayo kwa kufanya kazi mbalimbali ili tupate mkate wa leo na kesho. Huu ni msamiati wa watu wanaofanya kazi mbalimbali : 1. Dobi : Hufanya kazi ya kuosha nguo 2. Karani : Anayeangalia matumizi ya pesa katika benki au kampuni fulani 3. Katibu : Anayeweka rekodi za mambo na orodha mbalimbali katika kampuni au idara fulani 4. Kungwi : Hufunza vijana jandoni 5. Mchuuzi : Anayeuza bidhaa kutoka nyumba hadi nyumba 6. Mfinyanzi : Hufinyanga udongo kutengeza vyombo kama vyungu, n.k 7. Mhandisi : Anayefanya kazi ya kuunda au kurekebisha injini/mashine mbalimbali 8. Mhasibu : Mtu anayefanya kazi ya hesabu 9. Muhunzi : Hufua vyuma 10. Mkutubi : Anayeweka rekodi za vitabu katika maktaba, na kuwasaidia wanaotaka kuomba vitabu. 11. Tabibu : Anayetibu watu, daktari 12. Topasi : Kazi ya kuosha vyoo. |