09-02-2021, 07:28 AM
KISWAHILI 1
Soma kwa makini shairi lifuatalo kisha jibu maswali yanayofuata.
Tendawili: Tega: Mtalitegua leo?
Oneni mazinge ya njia, enyi mbele mwendao,
Msizimwe macho na vumbi la pofuo,
Msizibwe masikio na upepo uvumao,
Msizibwe pua na mnuko unukao,
Oneni majani ya upepo huu uvumao.
Tafiti chanzo na midundo ya yote yapitayo:
Anzia kijijini huko kwa mtu – kwao,
Watu huko watakwambia hali yao,
Huko, utenzi wa dhiki ndio uimbwao,
Utawaona wamekabwa koo zao,
Ngoma si ya furaha ichezwayo leo,
Bei ya vitu hupanda, sio bei ya mazao,
Na maisha yamepanda, sio maisha yao.
Njoo kwa wafanyakazi – mali wazalishao,
Watakweleza haki ikabwavyo koo,
Ukemi umezidi – ahaa! Siyo vilio,
Bei ya vitu hupanda, siyo mshahara wao,
Wafaidio ni wale wenye vyeo,
Yasikilize kidogo mazungumzo yao:
“Tutakutana wapi – New Afrika – leo?
“Palm Beach. New Afrika pamechosha, siyo?
Hizi ni enzi za wenye nafasi zao,
Asiye na fedha katu hana bao,
Na wasio na bao hulia kikwao.
Au tuyamulike mashule tuliyo nayo,
Wanafunzi – habari zafika kila leo,
Kiboko cha nidhamu ni halali yao,
Kila wapazapo sauti zao,
Hupigwa konzi na walimu wao,
Na wengine hurudishwa kwao.
Enyi wenye kuona, yapi yale muonayo,
Kulikucha, kulikucha au uongo huo?
Walenge, walengao, wafume wafumao,
Lugha ya mata itasemwa, siyo?
Oneni mazinge ya njia, enyi mbele mwendao,
Uko wapi mwanga wa mwenge umulikao,
Tariki ya ndoto yetu tuiotayo?
Hata hivyo, washairi tunao,
Na kila siku hupaza sauti zao,
Tendawili hili litateguliwa leo?
MASWALI
(a) Andika kichwa kifaacho kwa shairi ulilosoma
(b) Toa maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi.
(i) Tariki
(ii) Ukemi
(iii) Vumbi la pofuo
(iv) Konzi
(v) Katu
© Mwandishi anazungumzia nini katika ubeti wa tatu na wa tano? Toa hoja mbili kwa kila ubeti.
(d) Mwandishi ana maana gani anaposema “utenzi wa dhiki ndio uimbwao” katika ubeti wa pili?
SWALI 2
MAJIBU YA SWALI LA 1
(a) Kichwa cha shairi kiandikwe kwa herufi kubwa na kisizidi maneno matano (5)
Mf: – KITENDAWILI
(b) Maana ya maneno
(i) Tariki – njia
(ii) Ukemi – ukulele, sauti ya juu sana ya mtu au kitu, yowe, maneno makali ya kukaripia anayosema mtu
(iii) Vumbi la pofuo – vumbi linalomfanya mtu kupoteza uwezo wa macho yake kuona.
(iv) Konzi – vidole vya mkono uliokunjwa pamoja kwa lengo la kumpiga mtu kichwani
© Ubeti wa tatu
Mwandishi anazungumzia yafuatayo:
(d) Mwandishi anamaanisha yafuatayo:
– Kutokana na hali ya maisha basi kila lisemwalo na jamii huwa limebeba hali halisi ya maisha ya shida yanayoikabili jamii husika.
SWALI LA 2
Hapa unapaswa kufupisha shairi hilo kinathari kwa kuzingatia yafuatayo:
ZINGATIA PIA
NB: Ufupisho huwa theluthi moja (1/3) ya habari ya awali.
JINSI YA KUJIBU MASWALI YA SEHEMU A : UFAHAMU NA UFUPISHO
SWALI LA 1Soma kwa makini shairi lifuatalo kisha jibu maswali yanayofuata.

- Fupisha shairi ulilosoma kwa maneno yasiyozidi mia na hamsini (150) na yasiyopungua mia moja (100).
MAJIBU YA SWALI LA 1
(a) Kichwa cha shairi kiandikwe kwa herufi kubwa na kisizidi maneno matano (5)
Mf: – KITENDAWILI
(b) Maana ya maneno
(i) Tariki – njia
(ii) Ukemi – ukulele, sauti ya juu sana ya mtu au kitu, yowe, maneno makali ya kukaripia anayosema mtu
(iii) Vumbi la pofuo – vumbi linalomfanya mtu kupoteza uwezo wa macho yake kuona.
(iv) Konzi – vidole vya mkono uliokunjwa pamoja kwa lengo la kumpiga mtu kichwani
- Kitenzo cha kupigwa
© Ubeti wa tatu
- wafanyakazi kukosa haki yao wakati wao ndio wazalishaji.
- hakuna uwiano kati ya bei ya vitu inavyopanda na mishahara ambayo haijapandishwa.
- Wenye vyeo ndio wenye pesa na wanaofaidi maisha kwani hata wanabadilisha sehemu za kustarehe.
- Wasio na nafasi hata kukosa fedha hawana la kufanya
Mwandishi anazungumzia yafuatayo:
- Anawasemea wananchi wanaoona uozo unaoendelea katika jamii na hawawezi kusema
- Anajua mwenge wa uhuru uliwekwa ili kumulika waovu sasa maovu yapo ndani ya jamii. Mwenge ufanye kazi yake, yaani viongozi wenye dhamana wasimame kwenye nafasi zao kuondoa maovu hayo
- Anawaasa washairi wawe wazi kusema kweli ili jamii iwe huru
(d) Mwandishi anamaanisha yafuatayo:
– Kutokana na hali ya maisha basi kila lisemwalo na jamii huwa limebeba hali halisi ya maisha ya shida yanayoikabili jamii husika.
SWALI LA 2
Hapa unapaswa kufupisha shairi hilo kinathari kwa kuzingatia yafuatayo:
- Mawazo makuu
- Watu/wananchi wawe macho kulingana na maisha ambayo si mazuri
- Chanzo cha maisha magumu – ni bora kuangalia/kufanya utafiti kuanzia vijijini. Watu wanaishi maisha ya dhiki
- Mijini wafanyakazi ndio wanaozalisha lakini hawana haki
- Kupanda kwa bidhaa na huku mishahara ikidumaa huongeza adha ya maisha
- Wenye navyo wanafaidi maisha kuliko wasio navyo
- Maisha ya shuleni – wanafunzi hawana nafasi ya kutoa mawazo yao
- Mwenge wa uhuru umulikao ufanye kumulika na kuondoa uozo wote.
ZINGATIA PIA
- Mpangilio mzuri wa hoja wenye ufasaha wa lugha
- Tumia maneno yako mwenyewe bila kupotosha maana ya msingi
- Zingatia taratibu za uandishi na mpangilio wa aya
- Zingatia idadi ya maneno uliyopewa
NB: Ufupisho huwa theluthi moja (1/3) ya habari ya awali.
Mwl Maeda