JINSI YA KUJIBU MASWALI YA SEHEMU A : UFAHAMU NA UFUPISHO - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Sekondari (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=4) +---- Forum: Kidato cha tano na sita (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=44) +----- Forum: Maswali na majibu (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=47) +----- Thread: JINSI YA KUJIBU MASWALI YA SEHEMU A : UFAHAMU NA UFUPISHO (/showthread.php?tid=1103) |
JINSI YA KUJIBU MASWALI YA SEHEMU A : UFAHAMU NA UFUPISHO - MwlMaeda - 09-02-2021 KISWAHILI 1 JINSI YA KUJIBU MASWALI YA SEHEMU A : UFAHAMU NA UFUPISHO
SWALI LA 1Soma kwa makini shairi lifuatalo kisha jibu maswali yanayofuata. Tendawili: Tega: Mtalitegua leo? Oneni mazinge ya njia, enyi mbele mwendao, Msizimwe macho na vumbi la pofuo, Msizibwe masikio na upepo uvumao, Msizibwe pua na mnuko unukao, Oneni majani ya upepo huu uvumao. Tafiti chanzo na midundo ya yote yapitayo: Anzia kijijini huko kwa mtu – kwao, Watu huko watakwambia hali yao, Huko, utenzi wa dhiki ndio uimbwao, Utawaona wamekabwa koo zao, Ngoma si ya furaha ichezwayo leo, Bei ya vitu hupanda, sio bei ya mazao, Na maisha yamepanda, sio maisha yao. Njoo kwa wafanyakazi – mali wazalishao, Watakweleza haki ikabwavyo koo, Ukemi umezidi – ahaa! Siyo vilio, Bei ya vitu hupanda, siyo mshahara wao, Wafaidio ni wale wenye vyeo, Yasikilize kidogo mazungumzo yao: “Tutakutana wapi – New Afrika – leo? “Palm Beach. New Afrika pamechosha, siyo? Hizi ni enzi za wenye nafasi zao, Asiye na fedha katu hana bao, Na wasio na bao hulia kikwao. Au tuyamulike mashule tuliyo nayo, Wanafunzi – habari zafika kila leo, Kiboko cha nidhamu ni halali yao, Kila wapazapo sauti zao, Hupigwa konzi na walimu wao, Na wengine hurudishwa kwao. Enyi wenye kuona, yapi yale muonayo, Kulikucha, kulikucha au uongo huo? Walenge, walengao, wafume wafumao, Lugha ya mata itasemwa, siyo? Oneni mazinge ya njia, enyi mbele mwendao, Uko wapi mwanga wa mwenge umulikao, Tariki ya ndoto yetu tuiotayo? Hata hivyo, washairi tunao, Na kila siku hupaza sauti zao, Tendawili hili litateguliwa leo? MASWALI (a) Andika kichwa kifaacho kwa shairi ulilosoma (b) Toa maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi. (i) Tariki (ii) Ukemi (iii) Vumbi la pofuo (iv) Konzi (v) Katu © Mwandishi anazungumzia nini katika ubeti wa tatu na wa tano? Toa hoja mbili kwa kila ubeti. (d) Mwandishi ana maana gani anaposema “utenzi wa dhiki ndio uimbwao” katika ubeti wa pili? SWALI 2
MAJIBU YA SWALI LA 1 (a) Kichwa cha shairi kiandikwe kwa herufi kubwa na kisizidi maneno matano (5) Mf: – KITENDAWILI (b) Maana ya maneno (i) Tariki – njia (ii) Ukemi – ukulele, sauti ya juu sana ya mtu au kitu, yowe, maneno makali ya kukaripia anayosema mtu (iii) Vumbi la pofuo – vumbi linalomfanya mtu kupoteza uwezo wa macho yake kuona. (iv) Konzi – vidole vya mkono uliokunjwa pamoja kwa lengo la kumpiga mtu kichwani
© Ubeti wa tatu
Mwandishi anazungumzia yafuatayo:
(d) Mwandishi anamaanisha yafuatayo: – Kutokana na hali ya maisha basi kila lisemwalo na jamii huwa limebeba hali halisi ya maisha ya shida yanayoikabili jamii husika. SWALI LA 2 Hapa unapaswa kufupisha shairi hilo kinathari kwa kuzingatia yafuatayo:
ZINGATIA PIA
NB: Ufupisho huwa theluthi moja (1/3) ya habari ya awali. |