08-31-2021, 07:41 AM
MASWALI NA MAJIBU -5: DARASA LA 3 & 4
SEHEMU A: Chagua jibu sahihi
SEHEMU B: Jaza nafasi iliyoachwa wazi
MAJIBU
SEHEMU A: Chagua jibu sahihi
- Ipi kati ya sentensi hizi ni sentensi inayoonesha wakati ujao:-
- Kaka alichinja sungura jana. Sentensi hii ipo katika wakati gani?
- Badili kuwa hali ya mazoea, “Mkulima analima”……….
- Wingi wa neno kijiko ni………………………
- Baba …………..mama ni wazazi wangu.
- Wagonjwa wamelazwa…………………….
- Jua huchomoza asubuhi upande wa ………….
- Mtu ambaye hasikii huitwa……………..
- Samaki wa maji chumvi wana ……………nzuri.
- Vitabu ……….juu ya meza.
SEHEMU B: Jaza nafasi iliyoachwa wazi
- Umoja wa neno “mvi” ni……………
- Waislamu daima ………………kwenye misikiti.
- Andika neno moja tu kutokana na kundi hili. …………..(Machungwa, nyanya, ndizi, nanasi)
- Rehema ni bingwa wa……….mashairi (kughani, kugairi, kukubali)
- Hapo…………………za kale binadamu alifanana na sokwe. (mwanzoni, zamani, mwishoni, katikati)
- Mchwa huishi kwawingi na kuzaliana kwenye…………..(mzinga, zizi, kichuguu, kichukuu)
- Kamilisha methali hii:- Mvumilivu hula mbivu……………
- Toa maana ya nahau hii:- Kula chumvi nyingi…………….
- Tegua kitendawili hiki. Kila mtu humwabudu kila apitapo………….
- Andika kinyume cha neno baridi…………………..
Chakula bora ni muhimu sana kwa wagonjwa na hasa magonjwa ya muda mrefu kama vile UKIMWI, kifua kikuu na saratani. Mgonjwa anayekula vizuri, dawa hufanya kazi vizuri. Lishe bora kwa kweli, ndiyo dawa ya magonjwa kwa sababu mwili hujenga kinga.
Mtu asiyekula chakula cha kujenga mwili ni sawa na kujenga nyumba isiyo imara ambayo wakati wowote inaweza kubomoka.
- Dawa bora ya wagonjwa ili waweze kujenga kinga za mwili ni …………
- Magonjwa ya muda mrefu yaliyotajwa katika habari hii ni…………..
- Dawa hufanya kazi vizuri zaidi kwa………………
- Mtu aliyekula chakula cha kujenga mwili ni sawa na………..
- Mwandishi amesema katika habari kuwa chakula bora ni muhimu kwa……
MAJIBU
- A
- A
- B
- B
- D
- B
- A
- C
- B
- A
- Mvi
- huswali
- matunda
- kughani
- zamani
- kichuguu
- mbivu
- kuishi miaka mingi
- mlango
- joto
- A
- C
- D
- B
- C
Mwl Maeda