MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - MASWALI NA MAJIBU -5: DARASA LA 3 & 4

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: MASWALI NA MAJIBU -5: DARASA LA 3 & 4
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
MASWALI NA MAJIBU -5: DARASA LA 3 & 4
SEHEMU A: Chagua jibu sahihi
  1. Ipi kati ya sentensi hizi ni sentensi inayoonesha wakati ujao:-
(a) zena atakuja kwetu (b) zena anakuja kwetu © zena alikuja kwetu (d) zena huja kwetu.
  1. Kaka alichinja sungura jana. Sentensi hii ipo katika wakati gani?
(a) uliopita (b) ujao © mazoea (d) uliopo
  1. Badili kuwa hali ya mazoea, “Mkulima analima”……….
(a) mkulima analima (b) mkulima hulima © mkulima alilima (d) mkulima atalima
  1. Wingi wa neno kijiko ni………………………
(a) majiko (b) vijiko © mavijiko (d) vikijiko
  1. Baba …………..mama ni wazazi wangu.
(a) ni (b) wa © ya (d) na
  1. Wagonjwa wamelazwa…………………….
(a) nyumbani (b) wodini © hodini (d) chumbani
  1. Jua huchomoza asubuhi upande wa ………….
(a) Mashariki (b) juu © magharibi (d) kulia
  1. Mtu ambaye hasikii huitwa……………..
(a) bubu (b) kiwete © kiziwi (d) kilema
  1. Samaki wa maji chumvi wana ……………nzuri.
(a) mabaka (b) ladha © chumvi (d) rangi
  1. Vitabu ……….juu ya meza.
(a) viko (b) vino © vimekaa (d) zipo
 
SEHEMU B: Jaza nafasi iliyoachwa wazi
  1. Umoja wa neno “mvi” ni……………
  2. Waislamu daima ………………kwenye misikiti.
  3. Andika neno moja tu kutokana na kundi hili. …………..(Machungwa, nyanya, ndizi, nanasi)
SEHEMU C: Chagua jibu sahihi kwenye mabano
  1. Rehema ni bingwa wa……….mashairi (kughani, kugairi, kukubali)
  2. Hapo…………………za kale binadamu alifanana na sokwe. (mwanzoni, zamani, mwishoni, katikati)
  3. Mchwa huishi kwawingi na kuzaliana kwenye…………..(mzinga, zizi, kichuguu, kichukuu)
SEHEMU D: Methali, Nahau na Vitendawili
  1. Kamilisha methali hii:- Mvumilivu hula mbivu……………
  2. Toa maana ya nahau hii:- Kula chumvi nyingi…………….
  3. Tegua kitendawili hiki. Kila mtu humwabudu kila apitapo………….
  4. Andika kinyume cha neno baridi…………………..
SEHEMU E:UFAHAMU: Soma habari ifuatayi kisha jibu maswali
Chakula bora ni muhimu sana kwa wagonjwa na hasa magonjwa ya muda mrefu kama vile UKIMWI, kifua kikuu na saratani. Mgonjwa anayekula vizuri, dawa hufanya kazi vizuri. Lishe bora kwa kweli, ndiyo dawa ya magonjwa kwa sababu mwili hujenga kinga.
Mtu asiyekula chakula cha kujenga mwili ni sawa na kujenga nyumba isiyo imara ambayo wakati wowote inaweza kubomoka.
  1. Dawa bora ya wagonjwa ili waweze kujenga kinga za mwili ni …………
(a) lishe bora (b) kuepuka magonjwa ya UKIMWI © kwinini (d) panado
  1. Magonjwa ya muda mrefu yaliyotajwa katika habari hii ni…………..
(a) Malaria na UKIMWI (b) kuharisha na Saratani © kifua kikuu, saratani na UKIMWI (d) UKIMWI, saratani na kwashakoo
  1. Dawa hufanya kazi vizuri zaidi kwa………………
(a) wagonjwa wa muda mrefu (b) kujenga nyumba bora © kukosa chakula bora (d) kula chakula bora
  1. Mtu aliyekula chakula cha kujenga mwili ni sawa na………..
(a) kufa haraka (b) kujenga nyumba isiyo imara © kukosa chakula bora (d) UKIMWI
  1. Mwandishi amesema katika habari kuwa chakula bora ni muhimu kwa……
(a) watoto (b) wanafunzi © wagonjwa (d) wazee
 
MAJIBU
  1. A
  2. A
  3. B
  4. B
  5. D
  6. B
  7. A
  8. C
  9. B
  10. A
  11. Mvi
  12. huswali
  13. matunda
  14. kughani
  15. zamani
  16. kichuguu
  17. mbivu
  18. kuishi miaka mingi
  19. mlango
  20. joto
  21. A
  22. C
  23. D
  24. B
  25. C