01-05-2022, 07:37 AM
Hino naswaha twajipa, Mbaruku ni amana
Tumwombe hatwendi kapa, Mola wetu Subhana
Awape na wasotupa, pengine wao hawana
Tupawapo si kuhepa, na mato kuyakodoa
Tumwombe Mola kwa hapa, mwenye sifa ziso doa
Awape na wasotupa, nao wapate kutoa
Ukipawa fanya pupa, wewe nawe kupeana
Si nofu hata kifupa, na Mngu atakuona
Atawapa wasokupa, na hali mutafanana
Tusijitie kishipa, kumfunzia Rabbana
Ukata kutoogopa, kupata ni kupanana
Awape wasiotupa, nao waanze kupana
Mkata hutapatapa, funguni simuondoe
Muombee kutokopa, Allaah amfungulie
Awape na wasokupa, ili na wao watoe
Wenye roho za kupapa, kijito kiwaepuke
Madeni wasiolipa, Mwenyezi awatunuke
Awape wasiotupa, hasadi iwaondoke
Sitaguwe wa kuwapa, Bwana Mngu si fakiri
Omba dua iso dupa, duwara iduru dori
Awape wasiotupa, kwani Mngu ni tajiri
Mohamed Khamis
Takaungu
18.01.2018
Tumwombe hatwendi kapa, Mola wetu Subhana
Awape na wasotupa, pengine wao hawana
Tupawapo si kuhepa, na mato kuyakodoa
Tumwombe Mola kwa hapa, mwenye sifa ziso doa
Awape na wasotupa, nao wapate kutoa
Ukipawa fanya pupa, wewe nawe kupeana
Si nofu hata kifupa, na Mngu atakuona
Atawapa wasokupa, na hali mutafanana
Tusijitie kishipa, kumfunzia Rabbana
Ukata kutoogopa, kupata ni kupanana
Awape wasiotupa, nao waanze kupana
Mkata hutapatapa, funguni simuondoe
Muombee kutokopa, Allaah amfungulie
Awape na wasokupa, ili na wao watoe
Wenye roho za kupapa, kijito kiwaepuke
Madeni wasiolipa, Mwenyezi awatunuke
Awape wasiotupa, hasadi iwaondoke
Sitaguwe wa kuwapa, Bwana Mngu si fakiri
Omba dua iso dupa, duwara iduru dori
Awape wasiotupa, kwani Mngu ni tajiri
Mohamed Khamis
Takaungu
18.01.2018
Mwl Maeda