SHAIRI : AWAPE NA WASOTUPA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI : AWAPE NA WASOTUPA (/showthread.php?tid=2022) |
SHAIRI : AWAPE NA WASOTUPA - MwlMaeda - 01-05-2022 Hino naswaha twajipa, Mbaruku ni amana Tumwombe hatwendi kapa, Mola wetu Subhana Awape na wasotupa, pengine wao hawana Tupawapo si kuhepa, na mato kuyakodoa Tumwombe Mola kwa hapa, mwenye sifa ziso doa Awape na wasotupa, nao wapate kutoa Ukipawa fanya pupa, wewe nawe kupeana Si nofu hata kifupa, na Mngu atakuona Atawapa wasokupa, na hali mutafanana Tusijitie kishipa, kumfunzia Rabbana Ukata kutoogopa, kupata ni kupanana Awape wasiotupa, nao waanze kupana Mkata hutapatapa, funguni simuondoe Muombee kutokopa, Allaah amfungulie Awape na wasokupa, ili na wao watoe Wenye roho za kupapa, kijito kiwaepuke Madeni wasiolipa, Mwenyezi awatunuke Awape wasiotupa, hasadi iwaondoke Sitaguwe wa kuwapa, Bwana Mngu si fakiri Omba dua iso dupa, duwara iduru dori Awape wasiotupa, kwani Mngu ni tajiri Mohamed Khamis Takaungu 18.01.2018 |