11-28-2021, 05:59 PM
Njia zinazojitokeza katika uundaji wa msamiati ni kama ifuatavyo:
(iii) Miambatano kati ya jina tegemezi na jina huru. Jina tegemezi linatokana na kitenzi.Mwana + kwetu Mwanakwetu.
Njia ya kutumia mpangilio tofauti wa fonimu au vitamkwa: Kila lugha ina fonimu au sauti za msingi ambazo hutumika kujenga silabi ambazo nazo hujenga maneno yote ya lugha husika. Maneno mengi katika lugha huweza kupatikana kwa kubadili mpangilio wa vitamkwa/sauti-fonimu za lugha husika.
Kwa mfano:
Sauti-fonimu /a/, /o/, /n/ zikibadilishiwa mpangilio kwa namna mbalimbali zinaweza kuzalisha maneno kama vile:
(i) o-n-a => ona (ii) => noa (iii) => oana.
Njia ya miambatano
yaani kuunganisha maneno: Hapa maneno mawili yanaunganishwa na kuwa neno moja. Kuna aina mbalimbali za miambatano:
(i) Miambatano kati ya jina huru na jina huru.
mwana + hewa = mwanahewa
mwana + nchi = mwananchi
Afisa + misitu = Afisamisitu
(ii) Miambatano kati ya Nomino na Kivumishi.
Mla + mbivu = Mlambivu
(iii) Miambatano kati ya jina tegemezi na jina huru. Jina tegemezi linatokana na kitenzi.Mwana + kwetu Mwanakwetu.
Mpiga + maji Mpigamaji.
Mpiga + mbizi Mpigambizi
(iv) Miambatano kati ya kitenzi na jina.
Piga + mbizi pigambizi
Pima + maji pimamaji
Kutohoa maneno:
Kila lugha ina uwezo wa kuchukua maneno kutoka kwenye lugha nyingine ili kukidhi haja ya mawasiliano kulingana na maendeleo ya jamii. Kiswahili nacho kimechukua maneno kutoka lugha mbalimbali za kigeni na lugha za Kibantu na kuyatohoa ili kusadifu misingi ya sarufi yake.
Mfano:
(a) Kiingereza:
(i) tractro => trekta => trekita => terekita
(ii) plaugh => plau => pulau
(iii) shirt => sheti => shati
(iv) geography =>jiografia => jografia
(v) machine => mashine
(b) Kiarabu:
(i) laki => pokea
(ii) ahadi => milele
(iii) dhaifu => nyonge
(iv) ila => isipokuwa
© Kireno:
(i) bibo => bibo
(ii) roda => roda
(ii) mesa => meza
(iii) copa => kopa
(d) Kiajemi:
(i) bandar => bandari
(ii) dirisha => dirisha
(iii) kod => kodi
(iv) pilao => pilau.
(e) Kihindi:
(i) achari => achari
(ii) biyme => bima
(iii) ghati => gati
(iv) lakh => laki
(f) Kijerumani:
(i) schule => shule
(ii) hella => hela
(g) Kutoka Lugha za Kibantu
(i) faculty => kitivo <kipare/kisambaa.
(ii) composite => kivung <kipare
(iii) state house => ikulu <kigogo/kisukuma
(iv) national assembly => bunge<kigogo/kisambaa
(v) fluid => ugiligili <kinyakyusa
Njia ya urudufishaji:
Hii ni njia ya kurudia neno, likawa neon moja.
Mfano:
(i) kimbele => kimbele mbele
(ii) pole => pole pole
(iii) kinyume => kinyume nyume
(iv) kimya => kimya kimya
(v) kizungu => kizungu zungu
Kwa njia ya kufupisha maneno: Njia ya kufupisha maneno inachukua ama herufu ama silabi ya kwanza ya kila neno lililojitokeza katika jina zima la mahali au kitu funi.
Mfano:
(i) Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili => TUKI
(ii) Baraza la Kiswahili Tanzania => BAKITA
(iii) Chama Cha Mapinduzi => C.C.M
(iv) Baraza la Mitihani la Taifa => BAMITA
nk.
Njia ya kutumia mnyambuliko na uambishaji:
Neno jipya huundwa kwa kuunganisha viambishi kwenye mzizi au shina la neno. Njia hii hukuza lugha bila taabu kwani maneno ya lugha nyingi yanaweza kunyumbuliwa na kuambishwa, kama ifuatavyo:
(a) Mnyambuliko wa Majina:
(i) taifa => taifisha => taifishwa => taifishiwa. nk.
(ii) soma => somea => somesha => someshea => someshwa => someshewa => somesheka => , nk.
(b) Mnyambuliko wa Vitenzi:
(i) piga => pigana => pigisha => pigishwa => pigishia => pigia => pigiana, pigika, nk.
(ii) cheza => chezana => chezesha => chezeshwa => chezeshea => chezeana => chezwa => chezeka, nk.
© Mnyambuliko wa Vivumishi:
(i) fupi => fupisha => fupishia => fupishwa => fupishiwa => => fupishana => fupishika, nk.
(ii) safi => safisha => safishana => safishia => safishiana => safishika, nk.
(d) Mnyambuliko wa Vielezi:
(i) haraka => harakisha => harakishana => harakishika => harakishia => harakishiana, nk.
Njia ya Kutumia Uambishaji
(i) taifa => utaifa, mataifa, utaifishaji, nk.
(ii) piga => kupigana, anapiga, nk.
(iii) safi => msafi, wasafi, nk.
(iv) haraka => kuharakisha, nk.
Njia ya kufananisha sauti/umbo: Baadhi ya maneno ya Kiswahili yametokana na mwigo wa sauti au dhana ya kitu fulani.
Mfano:
(i) Piki-piki- piki-piki => pikipiki,
Neno ambalo limetokana na mwigo wa sauti (mlio) wa chombo husika.
(ii) tu-tu-tu => mtutu (wa bunduki)
neno ambalo limetokana na mwigo wa sauti ya risasi inapotoka kwenye bunduki baada ya kufyatuliwa.
(iii) kifaru
Hii ni zana ya kivita ambayo imepewa jina hilo kutokana na umbo lake lililofanana na mnyama aitwaye kifaru.
Njia ya vijenzi/viundaji:
Mara nyingi vijenzi huunda neno ambalo huwa nomino. Vijenzi hupachikwa mwishoni mwa kitenzi ili kiwe nomino. Maneno yanayojitokeza huwa na maana na ngeli tafauti tafauti.
Vijenzi vitumikavyo ni kama ifuatavyo:
Kijenzi Kitenzi Nomino
{i} jenga mjenzi
linda mlinzi
soma msomi
panda mpanzi
{ji} winda mwindaji
soma msomaji
sema msemaji
cheza mchezaji
linda mlindaji
{o} soma somo/masomo
sema msemo/misemo
cheza mchezo
{u} kua ukuu
tulia utulivu /mtulivu
tukuka utukufu/mtukufu
choka uchovu
{e} teua mteule
tuma mtume
kata mkate
umba kiumbe
MAREJELEO
Maganga (1997), OSW 102: Historia ya Kiswahili. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Masebo, J. A. Nyengwine, N. (2002), Nadharia ya Lugha ya Kiswahili, Kidato cha 5 na 6. Aroplus Industries Ltd: Dar es Salaam.
Nkwera, Fr. F. V. (2003), Sarufi, Fasihi na Uandishi wa Vitabu, Sekondari na Vyuo. Creative Prints Ltd: Dar es Salaam.
Mwl Maeda