01-06-2022, 07:59 AM
“OWENI WAKE WAWILI”
✏Oweni wake wawili
Au wanne kamili
Dada hawaihimili
Hali waliofikia.
✏Kila nyumba ina wari
Na wajane na vigori
Tupangeni mashauri
Twende kujichukulia.
✏Uma uko taabani
Na huku watu wazini
Hala hala ya jamani
Allah ameweka njia.
✏Wanawake wako wengi
Tena wapo kila rangi
Hili jambo la msingi
Lazima kufatilia.
✏Hebu tuokoe uma
Tuwaoe kina mama
Tuwafanyie huruma
Wapi watakimbilia.
✏Hal wao wakazini
Wapate kwenda motoni
Sie tuna kazi gani
Mijicho twawatolea.
✏Wana wake ni neema
Aliotupa Karima
Iko nyingi kwenye uma
Ni yetu masuulia.
✏Na dada waache wivu
Huo sio uwerevu
Wenzenu pao pakavu
Mume wajitafutia.
✏Leo hawa wasichana
Mara nne ya vijana
Yani wale wavulana
Nini watajifanyia.
✏Hapa leo yadhihiri
Hekima yake Ghafuri
Alipotoa amri
Ya wengi kujiolea.
✏Haya haya anzieni
Kuanzia thnateni
Haluwa isahanini
Na Shekhe kahudhuria.
✏Na thulatha na rubaa
Sikia ewe abaa
Madamu sio sabaa
Waweza kujiolea.
✏Tumwa ewaoa tisa
Na Mola alituasa
Kwamba yeye ni qabasa
Tuwe twamfatilia.
✏Ela Mola ehadidi
Kwenye uma Muhamadi
Wane wasiwe zaidi
Hekima yake Jalia.
Sheikh Juma Al Mazrui
✏Oweni wake wawili
Au wanne kamili
Dada hawaihimili
Hali waliofikia.
✏Kila nyumba ina wari
Na wajane na vigori
Tupangeni mashauri
Twende kujichukulia.
✏Uma uko taabani
Na huku watu wazini
Hala hala ya jamani
Allah ameweka njia.
✏Wanawake wako wengi
Tena wapo kila rangi
Hili jambo la msingi
Lazima kufatilia.
✏Hebu tuokoe uma
Tuwaoe kina mama
Tuwafanyie huruma
Wapi watakimbilia.
✏Hal wao wakazini
Wapate kwenda motoni
Sie tuna kazi gani
Mijicho twawatolea.
✏Wana wake ni neema
Aliotupa Karima
Iko nyingi kwenye uma
Ni yetu masuulia.
✏Na dada waache wivu
Huo sio uwerevu
Wenzenu pao pakavu
Mume wajitafutia.
✏Leo hawa wasichana
Mara nne ya vijana
Yani wale wavulana
Nini watajifanyia.
✏Hapa leo yadhihiri
Hekima yake Ghafuri
Alipotoa amri
Ya wengi kujiolea.
✏Haya haya anzieni
Kuanzia thnateni
Haluwa isahanini
Na Shekhe kahudhuria.
✏Na thulatha na rubaa
Sikia ewe abaa
Madamu sio sabaa
Waweza kujiolea.
✏Tumwa ewaoa tisa
Na Mola alituasa
Kwamba yeye ni qabasa
Tuwe twamfatilia.
✏Ela Mola ehadidi
Kwenye uma Muhamadi
Wane wasiwe zaidi
Hekima yake Jalia.
Sheikh Juma Al Mazrui
Mwl Maeda