SHAIRI: OWENI WAKE WAWILI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: OWENI WAKE WAWILI (/showthread.php?tid=2035) |
SHAIRI: OWENI WAKE WAWILI - MwlMaeda - 01-06-2022 “OWENI WAKE WAWILI” ✏Oweni wake wawili Au wanne kamili Dada hawaihimili Hali waliofikia. ✏Kila nyumba ina wari Na wajane na vigori Tupangeni mashauri Twende kujichukulia. ✏Uma uko taabani Na huku watu wazini Hala hala ya jamani Allah ameweka njia. ✏Wanawake wako wengi Tena wapo kila rangi Hili jambo la msingi Lazima kufatilia. ✏Hebu tuokoe uma Tuwaoe kina mama Tuwafanyie huruma Wapi watakimbilia. ✏Hal wao wakazini Wapate kwenda motoni Sie tuna kazi gani Mijicho twawatolea. ✏Wana wake ni neema Aliotupa Karima Iko nyingi kwenye uma Ni yetu masuulia. ✏Na dada waache wivu Huo sio uwerevu Wenzenu pao pakavu Mume wajitafutia. ✏Leo hawa wasichana Mara nne ya vijana Yani wale wavulana Nini watajifanyia. ✏Hapa leo yadhihiri Hekima yake Ghafuri Alipotoa amri Ya wengi kujiolea. ✏Haya haya anzieni Kuanzia thnateni Haluwa isahanini Na Shekhe kahudhuria. ✏Na thulatha na rubaa Sikia ewe abaa Madamu sio sabaa Waweza kujiolea. ✏Tumwa ewaoa tisa Na Mola alituasa Kwamba yeye ni qabasa Tuwe twamfatilia. ✏Ela Mola ehadidi Kwenye uma Muhamadi Wane wasiwe zaidi Hekima yake Jalia. Sheikh Juma Al Mazrui |