11-27-2021, 11:01 PM
Wafanyakazi
Wafanyakazi
Watu hawa hufanya kazi gani?
Kunazo kazi aina nyingi duniani.
Nyingine zinahitaji ujuzi, elimu na tajriba ya kiwango cha juu ukilinganisha na nyingine.
Mifano
- Mhasibu: Mtaalamu wa kuweka hesabu ya fedha.
- Mhandisi/injinia: Mjuzi wa kutengeneza, kuhudumia na kuunda mitambo.
- Tarishi/Katikiro: Anayehudumu ofisini kwa kutumwa kupeleka habari au ujumbe.
- Bawabu: Alindaye mlangoni.
- Topasi/chura: Asafishaye choo.
- Tabibu/daktari/mganga: Mwenye ujuzi wa kutibu.
- Muuguzi/mualisaji: Ahudumiaye wawele/wagonjwa
- Msarifu: Anayesimamia na kuidhinisha matumizi mazuri ya fedha katika shirika.
- Dereva: Aendeshaye vyombo vya nchi kavu k.v. gari
- Nahodha: Aendeshaye na kuongoza vyombo vya majini k.v. meli
- Rubani: Aendeshaye na kuongoza vyombo vya angani k.v.ndege
- Utingo/taniboi: Mpakiaji na mpakuaji wa mizigo katika gari.
- Hamali/mpagazi/mchukuzi: Abebaye mizigo kwa malipo.
- Machinga: Auzaye bidhaa rejareja kwa kuzungukazunguka.
- Malenga: Mtunzi stadi wa mashairi na nyimbo.
- Manju: Stadi wa kutunga na kuimba nyimbo katika ngoma.
- Kuli: Apakiaye na kupakua shehena za forodhani.
- Dobi: Afuaye na kupiga nguo za watu pasi kwa malipo.
- Sogora: Fundi wa kupiga ngoma.
- Saisi: Atunzaye wanyama wanaopandwa k.v. punda na farasi.
- Msajili: Awekaye orodha ya kazi, vitu au viumbe.
- Mkalimani/mtarijumani: Afasiriaye lugha moja hadi nyingine.
- Sonara: Atengenezaye mapambo kwa kutumia madini.
- Kinyozi: Anyoaye nywele.
- Msusi/msosi: Asukaye watu nywele.
- Ngariba: Apashaye wavulana tohara katika jando.
- Mkunga: Awasaidiaye wajawazito kujifungua.
- Kungwi: Afundishaye mwari wa kike au kiume.
- Mhariri: Asomaye, kusahihisha na kusarifu makala, magazeti n.k.
- Mshenga: Atumwaye kupeleka habari za ndoa (posa).
- Refa: Mwamuzi katika mchezo k.v. soka.
- Kasisi: Kiongozi wa kidini katika madhehebu fulani ya kikristo.
- Imamu: Kiongozi wa kidini katika madhehebu fulani ya kiislamu.
- Hakimu: Aamuaye kesi katika mahakama.
- Kadhi: Hakimu wa kiislamu.
- Mlariba: Akopeshaye wengine pesa.
- Mwekezaji: Anayeweka mali au pesa katika mradi au biashara.
- Meneja: Msimamizi au kiongozi katika kampuni au shirika.
- Karani: Afanyaye kazi ya kuandika k.m. barua na majarida.
- Kocha: Mwalimu wa mchezo k.v. soka.
- Mkutubi: Ahifadhiye vitabu maktabani na kuviazimisha.
- Mnajimu: Mwenye elimu ya nyota. Hutabiri mambo.
- Mpigaramli: Abashiriaye kwa kupiga bao.
- Mwajiri: Aandikaye mtu kwa kazi ya malipo au mshahara.
- Mzegazega: Achotaye maji na kuyauza.
- Dalali: Auzaye bidhaa katika mnada (soko la kushindania bei)
- Manamba: Mfanyikazi wa muda katika shamba kubwa.
- Mnyapara: Msimamizi wa kazi.
- Mhazili: Sekretari – Atunzaye barua na majarida na kuandika kwa mashine ofisini.
- Mhadhiri: Mwalimu katika chuo kikuu.
- Mwashi: Ajengaye nyumba kwa mawe.
- Mhunzi: Afuaye vitu vya madini ya chuma au bati.
- Seremala : Atengenezaye samani za mbao au miti.
- Mfinyanzi: Atengenezaye vyombo vya udongo k.m. vyungu.
- Mvuvi: Afanyaye kazi ya kuvua samaki.
- Mwanaanga: Afanyaye utafiti wa hali ya anga.
- Mkabidhi: Mtu atunzaye mali kwa ajili ya mwengine
- Diwani: Anayewakilisha watu wake katika serikali za wilaya
- Mzoataka: Anayeokota takataka
- Kaimu: Anayeshikilia cheo au wadhifa fulani kwa muda
Zoezi A.
Zitaje kazi za wafuatao.
- Mwalishi
- Sarahangi
- Mchuuzi
- Mwamizi
- Mfugaji
- Mamantilie
- Mlumbaji
- Mgema
- Mbunge
- Baharia
- Wakili
- Mjumu
- Diwani
- Mrumba
- Kandawala
- Gambera
- Taja watu wafanyao kazi hizi.
Aliyesomea diplomasia ni_________
Mtu afanyaye utafiti wa mambo ya sayari za juu__________
Mchezaji wa mpira wa miguu ni __________
Afanyaye kazi katika meli ni __________ .
Achezaye michezo ya riadha ni __________.
Raia anayejitolea kufanya kazi ya ulinzi ni __________
Askari katika jeshi la ulinzi __________
Anayeshughulika na sheria ni __________.
Maswali kadirifuMtu afanyaye utafiti wa mambo ya sayari za juu__________
Mchezaji wa mpira wa miguu ni __________
Afanyaye kazi katika meli ni __________ .
Achezaye michezo ya riadha ni __________.
Raia anayejitolea kufanya kazi ya ulinzi ni __________
Askari katika jeshi la ulinzi __________
Anayeshughulika na sheria ni __________.
Wafanyakazi
- Kamilisha majina ya wafanyakazi wanaoelewa.
- Mtu anayefua visu huitwa _____.
- Mtu aliye na elimu ya nyota huitwa _____.
- Mtu anayefua mabati na vyuma huitwa _____
- Daktari wa kuunganisha viungo vya mwili huitwa _____.
- Anayepakia na kupakua shehena bandarini huitwa _____.
- Mtu anayerusha ndege huitwa ____.
- Anayejenga nyumba kwa mawe, matofali au saruji huitwa _____.
- Msimamizi wa mabaharia huitwa _____.
- Fundi wa mitambo huitwa _____.
- Msimazi mkuu wa shamba huitwa _____.
- Mwizi wa baharani huitwa _____.
- Anayetengeneza pombe ya mnazi huitwa _____.
- _____ ni anayepeleka barua kwa posta.
- Mnunuzi katika mnada huitwa _____.
- Mtu anayewafunza vijana kunga za nyumbani huitwa _____.
- Anayehariri miswada huitwa _____.
- Mnunuzi katika mnada huitwa ____.
- Fundi stadi wa kupiga ngoma huitwa _____.
Watu hawa hufanya kazi gani?
- mrina
- mkimbizi
- katikiro
- manamba
- mwanazaraa
- mpagazi
- diwani
- meya
- mhazigi
- shaha
- msusi au msonzi
- msukaji
- seremala
- mdau au mshikadau
- saisi
- mswawidi
- mamantilie
- chokorido
- mhazili
Mwl Maeda