MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

MAJINA YA WATU KWA KAZI ZAO - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
MAJINA YA WATU KWA KAZI ZAO - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=9)
+--- Thread: MAJINA YA WATU KWA KAZI ZAO (/showthread.php?tid=1583)

MAJINA YA WATU KWA KAZI ZAO - MwlMaeda - 11-27-2021

Wafanyakazi
Kunazo kazi aina nyingi duniani.
Nyingine zinahitaji ujuzi, elimu na tajriba ya kiwango cha juu ukilinganisha na nyingine.
Mifano
  1. Mhasibu: Mtaalamu wa kuweka hesabu ya fedha.
  2. Mhandisi/injinia: Mjuzi wa kutengeneza, kuhudumia na kuunda mitambo.
  3. Tarishi/Katikiro: Anayehudumu ofisini kwa kutumwa kupeleka habari au ujumbe.
  4. Bawabu: Alindaye mlangoni.
  5. Topasi/chura: Asafishaye choo.
  6. Tabibu/daktari/mganga: Mwenye ujuzi wa kutibu.
  7. Muuguzi/mualisaji: Ahudumiaye wawele/wagonjwa
  8. Msarifu: Anayesimamia na kuidhinisha matumizi mazuri ya fedha katika shirika.
  9. Dereva: Aendeshaye vyombo vya nchi kavu k.v. gari
  10. Nahodha: Aendeshaye na kuongoza vyombo vya majini k.v. meli
  11. Rubani: Aendeshaye na kuongoza vyombo vya angani k.v.ndege
  12. Utingo/taniboi: Mpakiaji na mpakuaji wa mizigo katika gari.
  13. Hamali/mpagazi/mchukuzi: Abebaye mizigo kwa malipo.
  14. Machinga: Auzaye bidhaa rejareja kwa kuzungukazunguka.
  15. Malenga: Mtunzi stadi wa mashairi na nyimbo.
  16. Manju: Stadi wa kutunga na kuimba nyimbo katika ngoma.
  17. Kuli: Apakiaye na kupakua shehena za forodhani.
  18. Dobi: Afuaye na kupiga nguo za watu pasi kwa malipo.
  19. Sogora: Fundi wa kupiga ngoma.
  20. Saisi: Atunzaye wanyama wanaopandwa k.v. punda na farasi.
  21. Msajili: Awekaye orodha ya kazi, vitu au viumbe.
  22. Mkalimani/mtarijumani: Afasiriaye lugha moja hadi nyingine.
  23. Sonara: Atengenezaye mapambo kwa kutumia madini.
  24. Kinyozi: Anyoaye nywele.
  25. Msusi/msosi: Asukaye watu nywele.
  26. Ngariba: Apashaye wavulana tohara katika jando.
  27. Mkunga: Awasaidiaye wajawazito kujifungua.
  28. Kungwi: Afundishaye mwari wa kike au kiume.
  29. Mhariri: Asomaye, kusahihisha na kusarifu makala, magazeti n.k.
  30. Mshenga: Atumwaye kupeleka habari za ndoa (posa).
  31. Refa: Mwamuzi katika mchezo k.v. soka.
  32. Kasisi: Kiongozi wa kidini katika madhehebu fulani ya kikristo.
  33. Imamu: Kiongozi wa kidini katika madhehebu fulani ya kiislamu.
  34. Hakimu: Aamuaye kesi katika mahakama.
  35. Kadhi: Hakimu wa kiislamu.
  36. Mlariba: Akopeshaye wengine pesa.
  37. Mwekezaji: Anayeweka mali au pesa katika mradi au biashara.
  38. Meneja: Msimamizi au kiongozi katika kampuni au shirika.
  39. Karani: Afanyaye kazi ya kuandika k.m. barua na majarida.
  40. Kocha: Mwalimu wa mchezo k.v. soka.
  41. Mkutubi: Ahifadhiye vitabu maktabani na kuviazimisha.
  42. Mnajimu: Mwenye elimu ya nyota. Hutabiri mambo.
  43. Mpigaramli: Abashiriaye kwa kupiga bao.
  44. Mwajiri: Aandikaye mtu kwa kazi ya malipo au mshahara.
  45. Mzegazega: Achotaye maji na kuyauza.
  46. Dalali: Auzaye bidhaa katika mnada (soko la kushindania bei)
  47. Manamba: Mfanyikazi wa muda katika shamba kubwa.
  48. Mnyapara: Msimamizi wa kazi.
  49. Mhazili: Sekretari – Atunzaye barua na majarida na kuandika kwa mashine ofisini.
  50. Mhadhiri: Mwalimu katika chuo kikuu.
  51. Mwashi: Ajengaye nyumba kwa mawe.
  52. Mhunzi: Afuaye vitu vya madini ya chuma au bati.
  53. Seremala : Atengenezaye samani za mbao au miti.
  54. Mfinyanzi: Atengenezaye vyombo vya udongo k.m. vyungu.
  55. Mvuvi: Afanyaye kazi ya kuvua samaki.
  56. Mwanaanga: Afanyaye utafiti wa hali ya anga.
  57. Mkabidhi: Mtu atunzaye mali kwa ajili ya mwengine
  58. Diwani: Anayewakilisha watu wake katika serikali za wilaya
  59. Mzoataka: Anayeokota takataka
  60. Kaimu: Anayeshikilia cheo au wadhifa fulani kwa muda
Zoezi A.
Zitaje kazi za wafuatao.
  • Mwalishi
  • Sarahangi
  • Mchuuzi
  • Mwamizi
  • Mfugaji
  • Mamantilie
  • Mlumbaji
  • Mgema
  • Mbunge
  • Baharia
  • Wakili
  • Mjumu
  • Diwani
  • Mrumba
  • Kandawala
  • Gambera
  1. Taja watu wafanyao kazi hizi.
Aliyesomea diplomasia ni_________
Mtu afanyaye utafiti wa mambo ya sayari za juu__________
Mchezaji wa mpira wa miguu ni __________
Afanyaye kazi katika meli ni __________ .
Achezaye michezo ya riadha ni __________.
Raia anayejitolea kufanya kazi ya ulinzi ni __________
Askari katika jeshi la ulinzi __________
Anayeshughulika na sheria ni __________.
Maswali kadirifu
Wafanyakazi
  1. Kamilisha majina ya wafanyakazi wanaoelewa.
  2. Mtu anayefua visu huitwa _____.
  3. Mtu aliye na elimu ya nyota huitwa _____.
  4. Mtu anayefua mabati na vyuma huitwa _____
  5. Daktari wa kuunganisha viungo vya mwili huitwa _____.
  6. Anayepakia na kupakua shehena bandarini huitwa _____.
  7. Mtu anayerusha ndege huitwa ____.
  8. Anayejenga nyumba kwa mawe, matofali au saruji huitwa _____.
  9. Msimamizi wa mabaharia huitwa _____.
  10. Fundi wa mitambo huitwa _____.
  11. Msimazi mkuu wa shamba huitwa _____.
  12. Mwizi wa baharani huitwa _____.
  13. Anayetengeneza pombe ya mnazi huitwa _____.
  14. _____ ni anayepeleka barua kwa posta.
  15. Mnunuzi katika mnada huitwa _____.
  16. Mtu anayewafunza vijana kunga za nyumbani huitwa _____.
  17. Anayehariri miswada huitwa _____.
  18. Mnunuzi katika mnada huitwa ____.
  19. Fundi stadi wa kupiga ngoma huitwa _____.
 
Watu hawa hufanya kazi gani?
  1. mrina
  2. mkimbizi
  3. katikiro
  4. manamba
  5. mwanazaraa
  6. mpagazi
  7. diwani
  8. meya
  9. mhazigi
  10. shaha
  11. msusi au msonzi
  12. msukaji
  13. seremala
  14. mdau au mshikadau
  15. saisi
  16. mswawidi
  17. mamantilie
  18. chokorido
  19. mhazili