MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
UCHAMBUZI WA RIWAYA YA MWELE BIN TAABANI

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
UCHAMBUZI WA RIWAYA YA MWELE BIN TAABANI
#1
[Image: 19146291_1144818878955511_10198736487863...25x300.jpg]
KITABU: MWELE BIN TAABANI
MWANDISHI: MUDHIHIR MUDHIHIR
MWAKA : 2010
MWELE bin Taabani ni riwaya iliyoandikwa na kutolewa chapa ya kwanza mnamo mwaka 2010 ikiwa na malengo ya kuendeleza machahchari ya fasihi ya Kiswahili Afrika Mashariki. Mwandishi wa riwaya hii ni mheshimiwa Mudhihir Mohamed Mudhihir.
Mwele Bin Taabani ni riwaya maalumu yenye changamoto nzito kwa viongozi, watendaji, na wananchi katika mazingira duni ya dunia ya tatu. Mwandishi ametumia nahau, misemo, tashbiha, na msamiati tajiri wa lugha ya Kiswahili, Pia majina ya wahusika yaliyotumika katika riwaya hii huonesha kuakisi uhusiano wa jina na hulka za muhusika aliyekusudiwa katika nafasi fulani.
Katika riwaya hii mwandishi mheshimiwa Mudhihir Mohamed Mudhihir amegusia mambo yafuatayo
Mikorogo
Mwandishi amegusia suala la matumizi mabovu ya vipodozi kwani hivi sasa vipodozi vingi vinalenga kupoteza ngozi nzuri ya rangi nyeusi na watumiaji hudhani kwamba kuwa na rangi kama ya wamagharibi (weupe) basi ndio ataonekana binadamu zaidi kuliko yule ambaye amebaki kuwa na rangi yake halisi.
“Sodium azide (NaN3)”
“Sodium azide” ni kemikali mbaya sana! Tusilaumiane kuwa wazungu wanatuharibu na kuanza kuwanyoshea vidole kwamba wanaelekeza kila baya kwetu sisi.
Uongozi wetu nchini
Katika suala la uongozi wetu tunaona kwamba jinsi wanavyopigiana vikumbo na danadana, kanzu, tikitaka, tobo, chenga, na hatimaye wanakabana mpaka katika penati. Kwa hali kama hii ni nadra sana kusonga mbele katika maendeleo kwani kama wakubwa hawaelewani vema je, watoto watajisikiaje?
Mbunge wa jimbo la Kazamoyo mheshimiwa Chemka anasema “…mheshimiwa spika, sisi wananchi wa Kazamoyo tunaamini kuwa nasi tunayo haki sawa ya kupatiwa kipande chetu cha kitumbua cha taifa hili. Tumestahimili sana. Sasa tunasema wazi kuwa tumechoshwa na maisha haya ya uthakili”.
Ukahaba
Mwandishi amegusia suala la ukahaba katika maeneo mengi ya Mji Mkuu (mjini). Wasichana wadogo na hata wanawake waliostahili kuwa katika familia zao na kulea wanajihusisha na ukahaba. Mwandishi amekuwa mkweli kwa kuwa hali hi ya ukahaba ipo sana mji mkuu katika taifa la Wanakazamoyo.
Uteja
Mwandishi kupitia Wanakazamoyo anaonyesha kuwa uteja ni suala ambalo linazungumzwa sana na tena kwa lugha za kulaani na kukemea kwa nguvu sana lakini matokeo yake kuwa chanya ni ya kiasi kidogo.
Mateja huachwa tu bila kujua kuwa Wanakazamoyo wanapoteza nguvu kazi kutokana na wengi kuwa mateja na hivi kwamba ni ngumu kwa Wanakazamoyo kupata maendeleo kwa kiasi wanachokitaka.
Malezi
Mwandishi anaonyesha kuwa malezi ni jambo la muhimi sana ili kumuweka kijana katika hali ya kuwa na ujuzi zaidi katika kufanya kazi hata za nyumbani kama vile kusafisha vyombo ama kufua.
Mwandishi anaonyesha kuwa kijana aitwaye BaRaka bin Kitambi jinsi alivyolelelwa kizembe kiasi kwamba hata kufua nguo zake mwenyewe hawezi. Sasa hali kama hii jamani ni mbaya sana na hatutaisha kuwa kama bwana Jabali. Watoto walelewe katika misingi yenye kuwahimiza kufanya kazi.

Kasumba hasi

Watu wanaopangiwa maeneo fulani ya kufanya kazi hutoa visingizio vingi vyenye kasumba hasi kabisa. Ni sawa mazingira magumu, lakini je, wale unaodhani wako mazingira mazuri hawakumbani na changamoto za uongozi?
Tunaambiwa kuwa wauguzi hawapendi kwenda Kazamoyo kwa kuwa hakuna umeme, hakuna lami , hakuma kumbi za starehe, hakuna runinga, na mengine mengi.
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)