MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

MNYAMBULIKO WA VITENZI

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
MNYAMBULIKO WA VITENZI
#1
Mnyambuliko wa vitenzi ni jinsi vitenzi vinavyobadilika kulingana na kauli/hali mbalimbali. Kwa mfano kutokana na kitenzi ‘soma’ tunawezapata somea, somewa, somwa n.k. Ni vizuri kuelewa kwamba sio vitenzi vyote vinavyonyambulika katika kila kauli.
Kwa sasa tutaangalia kauli zifuatazo. Ili kuelewe kauli hizi vizuri, tutakutumia wewe kama mfano na mtu mwengine; lakini mnyambuliko unaweza kutumika kwa kitu chochote kile:
  1. [b]Kauli ya Kutenda[/b] – kitendo katika hali yake ya kawaida (bila kunyambuliwa)

  2. [b]Kauli ya Kutendea[/b] – kufanya kitendo kwa niaba(au kwa ajili) ya mtu mwengine

  3. [b]Kauli ya Kutendana[/b] – unamfanya mtu kitendo, naye anakufanya vivyo hivyo

  4. [b]Kauli ya Kutendena[/b] – unafanya kitendo kwa niaba mtu, naye anafanya kitendo hicho kwa niaba yako.

  5. [b]Kauli ya Kutendwa[/b] – kuathirika moja kwa moja na kitendo

  6. [b]Kauli ya Kutendewa[/b] – kitendo kufanywa kwa niaba yako au kwa ajili yako.

  7. [b]Kauli ya Kutendeka[/b] – kitendo kukamilika au kuwa katika hali timilifu

  8. [b]Kauli ya Kutendesha[/b] – kumfanya mtu atende jambo fulani

  9. [b]Kauli ya Kutendeshana[/b] – mtu anakufanya utende jambo fulani, nawe unamfanya atende jambo lilo hilo
     
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)