MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
WATANZANIA WALIOSHINDA TUZO YA KISWAHILI AFRIKA

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
WATANZANIA WALIOSHINDA TUZO YA KISWAHILI AFRIKA
#1

[Image: _99630718_e126acc3-862c-4a81-b390-6e209df8f4f7.jpg]
Dotto Rangimoto


Watanzania wawili
wametangazwa washindi wa Tuzo ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya
Afrika kwa mwaka 2017.
Wawili hao watazawadiwa
$5,000 kila mmoja katika sherehe ambayo itafanyika jijini Nairobi mwezi ujao.
Dotto Rangimoto alishinda kwenye kitengo cha ushairi kwa mswada wake Mwanangu
Rudi Nyumbani naye Ali Hilal Ali akashinda kitengo cha riwaya kwa
mswada wake wa Mmeza Fupa.
Waziri wa habari, utamaduni na Sanaa Tanzania Dkt Harrison Mwakyembe
amewapongeza wawili hao kwa ushindi huo na kusema ushindi wao “unachagiza
juhudi za serikali kuibidhaisha lugha ya Kiswahili.”
“Ushindi wa Watanzania hawa ni ushindi wa taifa kwa ujumla,” amesema
Dkt Mwakyembe kupitia taarifa.
Tuzo hiyo ilianzishwa mwaka 2014 na Dkt Lizzy Attree (Mkurugenzi wa Tuzo ya
Caine) na Dkt Mukoma wa Ngugi (Chuo Kikuu cha Cornell, Marekani), kwa lengo la
kuthamini uandishi kwa lugha za Kiafrika.
Aidha, tuzo hiyo inakusudiwa kuhimiza sanaa ya tafsiri baina ya lugha za
Kiafrika zenyewe kwa zenyewe, na pia kutafsiri maandishi ya lugha nyengine kwa
lugha za Kiafrika.
Wengine waliokuwa wanashindania tuzo hiyo ni: Mbaruk Ally – Hali Halisi (ushairi);
Hassan Omar Mambosasa – Nsungi (riwaya); Mwenda Mbatiah
– Kibweta cha Almasi (riwaya) na Richard Atuti Nyabuya – Umalenga
wa Nyanda za Juu (ushairi).
Majaji walikuwa Ken Walibora Waliaula (Mwenyekiti wa Majaji), mwanataaluma na
mwandishi; Daulat Abdalla Said, mwanataaluma na mwandishi, anayesomesha Chuo
Kikuu cha Taifa cha Zanzibar; na Ali Attas, mwandishi na mwalimu wa Kiswahili
na Kiingereza, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje, Japan.
“Mashairi yaliyomo katika diwani hii yametumiliwa lugha iliyojaa taswira
na majazanda yanayowakilisha vyema hisia zinazoelezwa katika dhamira
mbalimbali,” walisema majaji kuhusu diwani ya Mwanangu Rudi
Nyumbani.
“Mshairi amefaulu sana kuzitumia mbinu na miundo kadha wa kadha ili
kuyajadili maswala yanayohusu hali na mazingira tafauti tafauti katika maisha
ya binadamu. Anayazungumza maswala mazito mazito, lakini kwa namna ambayo
hayamuelemei msomaji wake.”
Walimsifu pia Bw Ali Hilal na kusema: “Si mno mtu kukutana na riwaya ya
Kiswahili ambayo mwandishi wake amejidhihirisha kuwa ni mbuji wa lugha fasaha
na ya kisanii, inayotiririka kitabia kwa hiari yake, na bila ya kuonesha dalili
zozote kwamba imelazimishwa.”
“Licha ya kwamba matukio ya riwaya hii yanatokea katika kisiwa cha kubuni,
maswala yanayojadiliwa humu ni miongoni mwa yale maswala sugu yanayoendelea
kulisumbua bara la Afrika kisiasa, kijamii na kiuchumi.”
Tuzo ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Kiafrika, yenye thamani ya
jumla ya Dola za Marekani 15,000, hutolewa kila mwaka kwa miswada bora, au kwa
vitabu vilivyochapishwa miaka miwili kabla ya mwaka wa kutolewa zawadi, katika
fani za riwaya, ushairi, wasifu na riwaya za picha.
Miswada inayoshinda huchapishwa na shirika la uchapishaji vitabu la East
African Educational Publishers (EAEP) na shirika la uchapishaji vitabu la Mkuki
na Nyota Publishers
Na mswada bora wa ushairi hufasiriwa kwa Kiingereza na kuchapishwa kitabu na
shirika la Africa Poetry Book Fund.
Tuzo hii inadhaminiwa na kampuni ya Mabati Rolling Mills, Kenya, na kampuni ya
ALAF Limited, Tanzania na pia Ofisi ya Makamu wa Mkuu wa Masuala ya Kimataifa
katika Chuo Kikuu cha Cornell, na Idara ya Taaluma za Afrika ya Chuo Kikuu cha
Cornell, Marekani.  CHANZO >>>>>>
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)