MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI: I LOVE YOU

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
SHAIRI: I LOVE YOU
#1
I LOVE YOU
Kizungu nimejaribu,
Nikwimbie mahabubu,
Ona ninapata tabu,
Nakupenda my dear!

Mwilini umezagaa,
Jina limetapakaa,
Usidhani chanjagaa,
Hadithi nasimulia!

Unanipa tabasamu,
Uliye wangu muhimu,
Mapenzi yako matamu,
Nashindwa kuhadithia.

Najiuliza maswali,
Huku nikiwaza mbali,
Na hivi silali sili,
Ai nimekuzimia!

Am sorry my dear,
Ikiwa nakusumbua,
Utenzi kukuimbia,
Upate kuninisia!

Sijui umeamka,
Au ungali kwa shuka,
Ewe ninaye kutaka,
Wake up my dear

Usidhani ni utani,
Vile naijua fani,
Unanitia jubuni,
Bila wewe ni udhia.

Sanga Sasa nanenepa,
Na kwako sitoki kapa,
Wanishika pale hapa,
Aah tamu nakwambia.

Na haya ndiyo mapenzi,
Kijana ninakuenzi,
Kupenda jina kitenzi,
Tupendane my dear.

Sasa nikwambie honey,
You are my number one,
Wengine naona nyani,
Bure kuning'ang'ania!

Ninatamani kutunga,
Ndefu beti kuzipanga,
But am not a singer,
Na muda unakimbia!

Siku nitakutungia,
Shairi tamu sikijia,
Usome lenye hisia,
Uanze kuniwazia!

Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704
Mwl Maeda
Reply
#2
KWA HERI YA BAIBAI
1. Penzi lako LA mgao, filieda halinifai,
Wape haohaohao, waombao kwa kudai, wape hao wafaao, baadaye wajidai,
Penzi limenikinai kwa heri ya kuonana.

2. Wagawa huko na huku, uombwapo hukatai!?
Washusha yangu shauku, na heshima haikai!
Nenda katafune kuku, tena na yake mayai,
Penzi limenikinai, kwa heri ya kuonana.

3. Unanipa dukuduku, haugawiki kwa pai!
Unaniona kapuku, unakana zangu rai,
Nimelifunga sanduku, sitaki unilaghai,
Penzi limenikinai, kwa heri ya kuonana.

4. Sikutaki sikutaki, naogopa vurumai,
Niache na yangu dhiki, hunidai sikudai,
Kwa kweli sikudhihaki, nimekwishakukinai,
Penzi limenikinai, kwa heri ya kuonana.

5. Kwa heri ya kuonana, kwa heri ya baibai,
Nenda kwa hao wa mana, wavaao suti tai,
Huko kwa wako mabwana mkale wali na chai,
Penzi limenikinai, kwa heri ya kuonana.

6. Kwangu usirudi tena, kwa vile huna madai,
Umeniumuza sana, kuchanganya hili tui,
Hakika nimeshaona, wewe kwangu ni adui,
Penzi limenikinai, kwa heri ya kuonana.

7. Nenda ukaneemeke, nakuombea uhai,
Bwana hao uwashike, mfike hata Dubai,
Ila kwangu usifike, kimwana kiruirui,
Penzi limenikinai, kwa heri ya kuonana.
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)