Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
SHAIRI: PIGENI KURA
#1
PIGENI KURA
Mshairi nimekwama, jamani pigeni kura,
Wanaume walalama, wanataka kunipora,
Wengi wao wanasema, wavutwa na yangu sura,
Jamani pigeni kura, madhara yasikute.

Mtunzi nagombaniwa, wa vitambi na vipara,
Sasa nachanganyikiwa, Nani kwangu ndiye bora?
Maneno nayoambiwa, tamu sio masihara,
Jamani pigeni kura, madhara yasinikute.

Kwa maneno ya kivuli, ataka aga kapera,
Ataka nimkubali, ndoa ikafjngwe mara,
Sasa mawazo ya mbali, nimezidiwa fikira,
Jamani pigeni kura, madhara yasinikute.


Abdul yule bwana, kijana mwenye kipara,
Zake mbinu nimeona, zenye janja na mikwara,
Hunitongoza kwa vina,  kumuacha ni hasara,
Jamani pigeni kura, madhara yasinikute.

Wasojua mashairi, mizani na mkarara,
Nao huongeza ari, hawachi jiparapara,
Sasa leo nimekiri, itanifika izara,
Jamani pigeni kura, madhara yasinikute.

Niseme nipate wote, yatanikuta madhara,
Nianze kutema mate, kutapika na kuhara,
Yangu hali iwe tete, ninyauke yangu sura,
Jamani pigeni kura, madhara yasinikute.

Nambieni nende wapi, kwao hao makapera,
Semeni bora ni kupi, nitakae mume bora,
Ikiwa raha hanipi, wangu moyo utafura,
Jamani pigeni kura, madhara yasinikute.

Siendi mbali nakoma, nawarushia mpira,
Hao wanoniandama, yupo nipate kisura?
Akili imenigoma, zimeniruka fikara,
Jamani pigeni kura, madhara yasinikute.

Filieda Sanga
Mama B
0753738704
Mwl Maeda
Reply
#2
HAINA HAJA YA KURA
Huko ni kunighusubu, shavu kunitia wembe,
Usinitie aibu, kunipanga na wakembe,
Huko utapata tabu, watakucheka wapambe,
Mimi pekee natosha, achana na visalata.

Mpaka tupige kura, ninashindana na nani?
Rama b ana Lana, Abdul maluuni,
Utahadhirika sana, usipokuwa mneni,
Hao wape kweli yao, njoo upike habibi.

Mola kakuumba hasa, mwendo wako kama nyati,
Maungoni una hisa, ni kama benki na noti,
Vile ukinesanesa, hali yangu mahututi,
Pajani na kwenye titi, laini kama yakuti.

Naimba nikupapase, pajani na kwenye titi,
Hilo wazi nikuase, mrembo mwenye bahati,
Niombacho usisuse mwenye laini sauti,
Fielida laazizi, nakuhitaji nyumbani.

Wallahi nimeamini, kwenye mwili huna shoti,
Maumgo yako laini, juu had I kwenye goti,
Njoo nikupe maraha, nikupende upendeke.

Ndembo anayo maudhi, hukojolea kabati,
Atashusha yako hadhi, hajui wewe ni siti?
Tena akuombe radhi, hawezi kwako kuketi,
Miye ndo dume la mbegu, chumba chetu meandaa.

Kuniweka kundi moja, na huyo mnuka shombo,
Miye naona mauja, utayaharibu mambo,
Wengine watakufuja, na atakunywesha tembo,
Njoo kwangu my darlying, aimaikize mlevi
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)