MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI: HERI KUU NNE

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
SHAIRI: HERI KUU NNE
#1
HERI KUU NNE:

Heri ya kwanza adhimu,
ya kutoa maarifa.
Kuwapa watu elimu,
wa karibu na masafa.
Hii ni heri muhimu,
isiyokuwa na ufa.
Heri kutoa ma'rifa,
kuliko kukaa kimya.

Ya pili nayo ni heri,
kuwa kimya abadani.
Maneno yenye hatari,
yasikutoke kinywani.
Ya nini kuleta shari,
kwa kauli za kihuni?
Heri mtu kuwa kimya,
kuliko kusema hovyo.

Na ipo heri ya tatu,
kuishi na watu wema.
Wanaojali ya utu,
matendo yenye huruma.
Wapenda watu si vitu,
ng'ang'ana nao daima.
Heri kuishi na wema,
kuliko kuwa pekeyo.

Heri ya nne ni bora,
kuwa kama gendaeka.
Anayetisha kwa sura,
makwao pori na nyika.
Ajabu siyo hasara,
pembeni ukajiweka.
Heri kuishi kivyako,
kuliko kuwa na mwovu.

©️ G. Gunguri
Chuo Cha Ualimu Mpwapwa
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)