MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
METHALI ZA KISWAHILI NA MAANA ZAKE KWA KINA

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
METHALI ZA KISWAHILI NA MAANA ZAKE KWA KINA
#1
METHALI ZA KISWAHILI NA MAANA ZAKE KWA KINA
  1. Adui wa mtu ni mtu
Methali hii inasisitiza juu ya tahadhari. Binadamu ni lazima awe na tahadhari sana katika kuenenda na maisha; ni lazima ajihadhari na kiumbe hiki binadamu. Kama vile binadamu alivyo na uwezo mkubwa wa kuhisi ndivyo pia alivyo na uwezo mkubwa wa kuathiri. Mtu ni mtu lakini si kila mtu ana utu. Utu ni ubinadamu na ubinadamu ni mwenendo mwema kwa binadamu wengine. Huo mwenendo mwema ni hiari na matakwa ya huyo mwenyewe. Hiari ni siri ya moyo. Kila mtu ana moyo wake. Kwa hiyo ana siri yake-hiyo aijuayo. Hiyo siri ya moyo wake yaweza kuwa njema au mbaya kwa mtu mwingine.Kwa hiyo kama vile ilivyo kweli kwamba adui yako aweza kuwa mwema wako ndivyo pia ilivyo kweli kwamba mwema wako aweza kuwa adui yako.
  1. Aliye kando haangukiwi na mti
Hii ni methali nyingine ambayo yamtaka mwanadamu awe mwangalifu zaidi awe na tahadhali. Mti ni mti, na huumiza hasa umuangukiapo kiumbe kama binadamu. Kwa hiyo binadamu akiuelewa huo udaifu wake na kama anataka kuishi maisha marefu zaidi, anawajibika kusimama kando ili mti usimuangukie. Maana inayojitokeza hapa ni kwamba tusijitie katika mambo yasiyotuhusu au tusiyoyaweza. Ni lazima tuchunguze uhusiano na uwezo wetu kabla hatujaamua kujishirikisha katika mambo ya wenzetu. Kama tukibaini kwamba mambo hayo hayatuhusu, hatuyawezi au yanaweza yakatuletea madhara, basi tukae kando na tuwaachie wenyewe waendelee na mambo yao.
  1. Dawa ya moto ni moto
Methali hii inajulikana sana kwa matumizi yake ya kila siku. Ni wazi kuwa ukitaka kukinga moto ambao unakuja basi nawe yakubidi uwashe moto. Hii hutumika kwenye vijiji vilivyo karibu na mapori. Maana ya methali hii hasa ni kwamba ubaya dawa yake ni ubaya vilevile. Yaani akufanyiaye mabaya basin awe mfanyie mabaya.Hivyo ubaya huo ukikutana aidha kutatokea namna Fulani ya usuluhisho. Tafsiri nyingine ya methali hii ni kwamba jambo lolote tukiona laenda kombo basi twatakiwa kuwahi kulitibu kabla halijawa baya.
  1. Fimbo ya jirani haiwezi kuua nyoka
Methali hii inafanana na ile isemayo hamadi kibindoni. Huwezi kufanya jambo kwa kutegemea msaada kutoka sehemu nyingine (jirani). Jirani hawezi kutatua matatizo yako kama vile ambavyo wewe mwenyewe ungeyatatua. Jirani si wa kutegemea. Twahitajika kujitegemea wenyewe kuliko kutegemea wengine.
  1. Fimbo ya karibu ndio iuayo nyoka
Ni kweli kwamba fimbo iliyo karibu ndiyo iwezayo kuua nyoka. Methali hii hutumiwa wakati unapoongelea jambo ambalo utatuzi wake watakikana haraka ama pengine bila kupata msaada sehemu nyingine. Msaada wowote, akiba yoyote ambayo ipo tayari kwa wakati unaotakiwa, ndio msaada pekee unaothaminiwa na kutambuliwa. Huwezi kutegemea kitu ambacho kiko mbali ama kukipata kwake kuna matatizo ikilinganishwa na kitu ambacho kipo tayari kihitajiwapo.
  1. Hata kiporo ni ugali
Methali hii hutumiwa kwa kusema kuwa kwa kweli kula ni kula. Hakuna chakula ambacho hakina umuhimu. Chakula ni chakula hata kikiwa kiporo.
  1. Karamu mbili zilimshinda fisi kuzila
Methali hii yatutahadharisha tusiwe wenye tamaa tama. Twaambiwa kuwa unapokuwa na haja ya jambo Fulani ukawa katika hali ya kutekeleza basi usirukie jambo jingine la aina ile ile maana waweza ukakosa huku na kule. Shika ulichoshika usifuate kile ambacho huna uhakika wa kukipata.
  1. Kauli nzuri ni bora kuliko mali Hakika kauli nzuri ni kweli kwamba ni bora kuliko utajiri. Hivyo ulimi kwa kweli kutokana na methali hii ni kitu cha kuchunga sana. Kabla hatujasema neno lolote twahitajiwa kuchuja na kuhariri yale tunayotegemea kusema kabla ya kusema, maana neno likishasemwa ni vigumu kufutika kwani lilishasikika.
  2. kifo hukaa kwenye mshipi
Hapa mshipi umetumiwa kama kielelezo tu. Maana hasa ya methali hii ni kwamba binadamu tunapotembea tusijione kuwa ni kitu sana. Yatupasa kufahamu kuwa kila tunapotembea kifo kinatuzunguka.
  1. Kila mjinga ana manufaa yake
Haiwezekani mtu awe mjinga moja kwa moja. Kuna siku anaweza kufanya mambo mazuri watu wakashangaa.Watu wengine huamini kuwa hakuna ujinga ambao ndani yake hauna welevu. Hivyo tusije tukawadharau watu kuwa ni wajinga na tukaamini hivyo moja kwa moja.Tukifanya hivyo tutakuwa tunafanya makosa.
  1. Kilichokatwa na shoka hupotea lakini kilichokatwa na mdomo hakipotei
Ni wazi kwamba shoka linapokata daima hukata vitu ambavyo vyaweza kupotea. Kinachokatwa na mdomo aghlabu hakipotei, maanachaenda tumboni. Binadamu anapokata kitu kwa mdomo ni wazi kuwa baadaye hukila kitu hicho na kwamba kitamnufaisha katika kujenga, kulinda na kuhifadhi mwili. Methali hii yatushauli kuwa tufanye mambo yetu kwa dhamiri maana katika dhamiri kuna mafanikio. Tusifanye mambo juu juu tu ; bali kwa undani na dhati.
  1. Kitanda usichokilalia hujui kunguni wake
Si rahisi kufahamu kunguni wa kitanda usichokilalia wanauma kiasi gani. Hivyo anayelalia kitanda hicho ndiye anayefahamu kunguni wake.Kimatumizi methali hii inatueleza kuwa mtu hawezi kujua shida zinazompata mtu mwingine.Jambo lisilokuhusu ama kukupata huwezi kujua ubaya wake.
  1. Kuishi na ndugu ni kuvumiliana
Methali hii inajieleza yenyewe. Ndugu wana tabia mbalimbali na nyingi ya tabia za ndugu ni kinyume cha vile ambavyo tungewatazamia wawe. Hivyo basi unapoamua kukaa na ndugu basi yakubidi uwe mvumilivu kwani vitendo vingine vyaweza kuwa vya kusikitisha na kutisha. Hivyo basi tunapoamua kukaa na ndugu lazima tuwe wavumilivu wa maovu yote ambayo watatufanyia.
  1. Macho mengi huona kuliko moja
Uwingi daima ni bora maana una nguvu. Macho mawili ni bora zaidi kuliko bora. Umoja na ushirikiano ni ngao imara kabisa katika maisha. Katika umoja kuna ushirikiano na katika ushirikiano kuna mafanikio.
  1. Maji marefu muulize chura
Chura kwa kawaida huishi majini. Twategemea kwamba ayajua vema mazingira yake. Kama ndivyo, basi yumkini afahamu urefu na ufupi wa maji. Yafaa kwa muogeleaji kutafuta ushauri wa chura hata kabla ya kuyazama maji. Ili tuufahamu undani na ukweli wa jambo yatubidi daima tufanye uchunguzi utakiwao. Njia mojawapo ya kuchunguza ni kuwauliza na kutaka ushauri wa hao wahusikanao na jambo hilo. Kuuliza ni kufahamu.
Methali nyingine :
  • Maji yanayokuja kwa nguvu yape njia yapite
  • Mali ni sawa na maua
  • Maneno ya kaburini huishia kaburini
  • Masikini halali mchana
  • Maziwa ya ng′ombe wa kuazima yanywe huku ukisimama • Kidole kimoja hakivunji chawa
  • Kizuri chajiuza kibaya chajitembeza
  • Apewaye ndiye aongezwaye
  • Haraka haraka haina Baraka
  • Mchagua jembe si mkulima
  • Mwenye kovu usidhani kapoa
  • Kutoa ni moyo usifikiri ni utajiri
  • Bura yangu sibadili na rehani
  • Chovya chovya humaliza buyu la asali
  • Jungu kuu halikosi ukoko
  • Chanda chema huvikwa pete
  • Umleavyo ndivyo akuavyo
  • Mganga hajitibu mwenyewe
  • Mgonjwa haulizwi dawa
  • Mcheka janga halijampata
  • Kunguru mwoga hukimbiza bawale
  • Debe tupu haliachi kuvuma
  • Maji na hata yachemke vipi hayasahau kwao baridi
  • Mtka cha uvunguni shariti ainame
  • Ivute ngozi ingli bichi
  • Samaki mmoja ameoza wote wameoza
  • Dalili ya mvua ni mawingo
  • Mwanamke mzuri hakosi kilema
  • Mwenye macho haambiwi tazama
  • Zimwi likujualo halikuli likakuisha
  • Mwendakwao haogopi giza
  • Ndege mjanja hulala juu ya mgude
  • Ndege mwenye maneno mengi hana nyumba
  • Ndovu hashindwi na pembe zake
  • Ng′ombe wa kwanza hanywi maji machafu
  • Njiwa huweza kuzaa mwewe
  • Nyama ya nundu huliwa na mfugaji
  • Palipo na mbuzi hapakosi wanambuzi
  • Palipo na kwale hapakosi mwingine
  • Penye vipofu wengi kengeza hufaidi
  • Simba mwenda kimya ndiye mla nyama
  • Ujirani mwema hutengeneza njia
  • Ukimfukuza sana mjusi hugeuka nyoka
  • Umande unaweza kuklunjiwa nguo lakini mvua haiwezekani
  • Ukubwa si mali
  • Watu hukataza tonge lakini sio mdomo
  • Wema huzaa wema
  • Vita havina macho
  • Utamu wa kidonda unamuua nzi
  • Utajiri ni kama umande
  • Usitukane wakunga uzazi ungalipo
  • Usivuke maji usiyoweza kuyaoga
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)