MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

Matumizi ya Lugha Katika Ushairi na Vipengele Vyake

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
Matumizi ya Lugha Katika Ushairi na Vipengele Vyake
#1
Maelezo yametolewa na wataalamu kuhusu matumizi ya lugha katika ushairi ambayo pia yanatupa mwelekeo ufuatao:
Gibbe (1998) anasema kuwa lugha ya ushairi huwa ya muhtasari na mkato kwa matumizi ya mizungu kama vile inkisari na mazida. Lugha hii pia ina mpangilio tofauti unaochochewa na idhini waliyonayo washairi (Wamitila, 2006) na  (Syambo na Mazrui, 1992). Idhini hii inachangia ukiushi mwingi katika ushairi kama ule wa kisarufi, kihijai, kisemantiki na awamu ya historia (Wamitila, 2006).
Syambo na Mazrui (1992), Wamitila (2006), King’ei na Kemoli (2001) na Massamba (1983) wanataja kipengele cha tamathali za usemi kama sehemu muhimu katika suala la matumizi ya lugha katika mashairi. Mifano ya tamathali za usemi zitumikazo katika ushairi ni tashihisi, tashibiha, taswira, sitiari, kinaya, takriri na taashira (Kisia na Mwarandani, 2007).
Maelezo ya hawa wataalamu yanatupa ruwaza nzuri ya vipengele vya lugha vya kuzingatia unapochambua lugha katika mashairi. Mbali na lugha ya ushairi kuwa ya mkato, ukiushi mwingi na tamathali za usemi, lugha hii pia, kwa mujibu wa Syambo na Mazrui (1992), huchanganya msamiati wa kigeni kama vile Kiarabu ( hasa kwa mashairi yenye maudhui ya kidini) au wa lahaja. Lugha hii vile vile huwa na sifa za matumizi ya uwakilishi (Syambo na Mazrui, 1992) na pia sifa za uchimuzi, suala la utata, maneno ya kubuni na pia ya kikale (Wamitila, 2006).
Mulokozi na Kahigi (1979) wanaongezea matumizi mengine ya lugha katika mashairi kama vile kutumia misemo, methali na onomatopea. Mifano hii ya vipengele vya lugha ambavyo huweza kutumika katika mashairi inatupa nyenzo ambazo kwazo tunaweza kuibulia bayana hali halisi ya matumizi ya lugha katika ushairi wa.
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)