MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'BAHASHISHI'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'BAHASHISHI'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'BAHASHISHI'

Neno *bahashishi* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: i-/zi-*] yenye maana zifuatazo:

1. Kitu anachopewa mtu kama zawadi kwa kazi nzuri aliyoifanya.

2. Malipo ya ziada anayopewa mtu baada ya kupewa mshahara wake; nyongeza anayopewa mtu kama shukurani.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *bahashishi* limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu  *'bakhshiishi* *(soma: bakhshiishun/bakhshiishan/bakhshiishin  بخشيش)** yenye maana zifuatazo:

1. Malipo yatolewayo kwa mtu kama zawadi na Shukurani kwa kazi aliyoifanya. Kiarabu huitwa pia *ikraamiyyah إكرامية* pia *hadiyyah هدية.*

2. Malipo yatolewayo kwa mtu ili kumshawishi; rushwa.

3. Zawadi, hiba.

Kinachodhihiri ni kuwa neno *'bakhshiishun بخشيش* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *bahashihi* halikubadili maana zake katika lugha asili- Kiarabu.

*TANBIHI:*
Neno *bakhshiishun* linachukuliwa kuwa lahaja ya Kiarabu ya Kimisri na kwa Kiarabu Fasaha na Sanifu neno hili hutamkwa *baqshiishun بقشيش* kwa herufi *q* badala ya *kh* .

Etimolojia ya neno hili ni lugha ya Kiajemi ambapo lilipohamia katika lugha ya *ki-Turky* lilitamkwa *bahsis* na ndipo walipolichukua Waarabu wakati wa Utawala wa Ottoman.

Kwa Waturuki bahsis (bahashishi)  ilikuwa ni ada anayotoa mteja anapoingia sokoni kama ishara ya kuwashukuru wanaolihudumia soko kwa kuliweka katika hali ya usafi, kuvutia na kulisimamia vizuri.

Kisha maana ya *bahashishi* ikageuka kuwa zawadi, hiba na sadaka inayokuza mtangamano wa kijamii na kuchukuliwa kama ukarimu unaowasaidia wale wenye kipato kidogo.

Kadiri neno *bahshishi* ilipotamalaki likafungamana na utoaji wa huduma nzuri na ikawa ni kitu cha lazima na kuchukuliwa kuwa aina mojawapo ya rushwa.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)