MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

KIJUE KITABU KILICHOTUMIA MHUSIKA MMOJA TU

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
KIJUE KITABU KILICHOTUMIA MHUSIKA MMOJA TU
#1
Karibu katika KAMUSI.
KAMUSINI leo tunaangazia Wahusika katika Fasihi.
Makala ya kamusi inaeleza kwa ufupi ni kwa namna gani lugha humfinyanga muhusika wa kazi ya fasihi.
Tuanze hapa, Lugha ndicho kipengele mahususi ktk taaluma ya fasihi. Ndicho kifanyacho fasihi ijuzu na kukidhi vigezo vya kuwa sanaa.
Lugha ndiyo huyajenga maudhui. Maudhui hayo hufumbatwa na wahusika walio katika kazi ya fasihi.
Kariba, raghba na tajiriba zao huelezwa na lugha kisanaa na kisanii.
Wahusika kama viumbe bunilizi wa msanii huumbwa na kufinyangwa na lugha.
Lugha imfinyangayo muhusika fulani huwa imeteuliwa kwa indhari na tahadhari kubwa na fanani ajuaye kazi yake.
Aghalabu lugha hutumika ktk kumweleza muhusika kiasi cha kumpa hisi hadhira kupata hata taswira ya muhusika mawazoni na akilini.
Lugha humweleza muhusika ukubwa wake , udongo, unyonge , ukali, ucheshi wake, kariba zake, weledi , tajiriba , maarifa , nk. Yote haya hufanywa na lugha.
Kwa hiyo, umbo , taswira , picha za ukubwa wa muhusika fulani, umwamba, ukonki, ushenzi, ufirauni, ukatili, uzwazwa, ujuha , uzuzu , uzezeta , ujasiri , ujemedari , uzalendo , uwanaharakati, unafiki, wema, upendo, uadilifu, na nk yote hayo hufanywa na namna lugha inavyomwelezea muhusika fulani.
Lugha ikimweleza muhusika bila shaka hadhira inaweza kuamua kumtambua kama muhusika fulani kama muhusika mkuu, msaidizi, Kivuli, bapa, mjivuni, shujaa, mkwezwa, duara , kinara, nk.
Yote haya hutegemea ni kwa jinsi gani lugha ilivyotumika kumsana, kumuumba na kumfinyanga muhusika fulani ktk kazi ya fasihi.
Muhusika kupitia lugha inayotumika kumuumbia inaweza kuchagiza hadhira kumpenda au kumchukia , kumtoa maana ama kumfanya kiigizi, au kinyume chake muhusika fulani.
Wahusika huumbwa na lugha kisha wao pia hutumika lugha hiyo kuyajenga maudhui ya kazi ya fasihi.
Kwa hiyo, wahusika ndio sauti halisi ya msanii/ mtunzi / fanani wa kazi ya fasihi. Hadhira/ Msomaji au msikilizaji wa fasihi akipata hisia za ubaya au uzuri wa muhusika fulani kiasi cha kumwaga chozi ati kwa sababu Hurem Sultana ametawafu basi ujue mtumzi wa kazi hiyo amefanikiwa sana.
Ukisoma Tamthiliya ya NJE- NDANI kwa mfano utabaini ni kwa namna muhusika mmoja alivyoumbwa kisanaa na watunzi ameweza kuibeba Tamthiliya hiyo mwanzo hadi mwisho.
NJE- NDANI ndiyo Tamthiliya ya kwanza katika fasihi ya Kiswahili kutumia muhusika mmoja tu. ( Haijapata kutokea kabla hii).
NJE- NDANI sasa ipo Chuo Kikuu cha Dodoma, MuM , Jordan – Morogoro.
Tuandikie : majidkiswahili@gmail.com Au +255 715 83 84 80.
Majid Mswahili
Mchambuzi wa Lugha, Fasihi na Fasaha ya Kiswahili
11/06/2019.
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)