MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'BAIRI'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'BAIRI'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'BAIRI'

Neno *bairi* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: a-/wa-*] yenye maana ya *mnyama mkubwa mwenye nundu mgongoni abebaye mizigo wakati wa safari ndefu aghalabu jangwani; ngamia.*

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *bairi* limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu  *'baiiru*( *soma: baiirun/baiiran/bairiin بعير )* ambalo ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo:

1. Mnyama afaaye kumpanda kwa usafiri au kumbebesha mizigo miongoni mwa ngamia wa kiume na wa kike baada ya kutimia umri wa miaka minne.

2. Punda atumikaye kubeba mizigo.

Waarabu wana msemo maarufu: *Alba-aratu Tadullu Alal Baiiri البعرة تدل على  البعير*  kinyesi cha ngamia ni dalili ya kupita kwake hapo.

Kinachodhihiri ni kuwa neno *'baiirun بعير* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *bairi* lilichukua maana ya jumla ya mnyama *ngamia* na kuacha maana halisi ya mnyama aliyefikisha miaka minne akafaa kubeba watu na mizigo aghalabu kwa safari za jangwani.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)