MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'ALHAMISI'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'ALHAMISI'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'ALHAMISI'

Neno alhamisi  katika lugha ya Kiswahili ni Nomino [Ngeli: i-/zi-] yenye maana ya siku ya wiki iliyopo baina ya Jumatano na Ijumaa, siku ya nne ya wiki kuanzia Jumatatu.

Katika lugha ya Kiarabu neno alhamisi ( soma: alkhamiisu/alkhamiisa/alkhamiisi الخميس)  ni nomino yenye maana zifuatazo:

1. Sehemu moja ya kilichogawanywa sehemu tano.

2. Siku ya sita katika wiki iliyopo baina ya Jumatano na Ijumaa. (Hapa imezingatiwa wiki kuanza Jumamosi ili kuifanya Ijumaa ni siku ya mwisho wa wiki).

3. Moja ya siku za Pasaka, Alhamisi ya Pasaka Khamiisul Fisw-hi (Easther Thursday).

4. Jeshi linaloundwa na vikosi vitano Al-Jayshul Jarraru الجيش الجرار.

5. -enye urefu wa dhiraa tano aghalabu nguo.

Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu  alkhamisi الخميس lilipoingia  katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno alhamisi lilichukua maana ya siku ya wiki na kuziacha maana zingine.

TANBIHI:
Neno Alkhamisi katika Kiarabu lina maana ya siku ya tano kuanzia Jumapili ambayo kwa Kiarabu  inaitwa Al-Ahad الأحد yenye maana ya siku ya kwanza.

Katika Kiswahili kuna maneno mawili ambayo kilugha yana maana ya siku ya tano, moja likitajwa kwa neno lenye asili ya Kibantu (Jumatano) na lingine likitajwa kwa neno lenye asili ya Kiarabu (Alhamisi/Alkhamisi).

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 2 Guest(s)