MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'ALAMA'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'ALAMA'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'ALAMA'

Neno alama katika lugha ya Kiswahili ni Nomino [Ngeli: i-/zi-] yenye maana zifuatazo:

1. Mchoro au kitu kinachoashiria au kutambulisha kitu au jambo.

Mfano: Pete aliyoivaa ni alama ya upendo wa mumewe kwake.

2. Eneo dogo juu ya uso wa kitu kama vile nguo au ngozi lililosababishwa na jeraha, kidonda au lililowekwa kama pambo lenye rangi au sura tofauti na eneo linalolizunguka.

3. Athari iliyopo inayobainisha kitu au jambo lililokuwapo awali.

Mfano: Kovu ni alama ya kidonda.

4. Maksi anazopewa mwanafunzi kutokana na asilimia ya jumla ya maksi katika mtihani.

5. Kidokezo cha njia au kupita kwa kiumbe au chombo cha usafiri mahali.

Mfano: Tumekuta alama za nyayo za simba shambani.

6.Kiwakilishi cha maandishi kinachowekwa kwenye hati kuchukua nafasi ya saini ya mtu asiyeweza kuandika.

7. Kiashiria kinachodokeza kumbukumbu ya jambo au tukio lililopita.

Mfano: Mkuki wake umetiwa alama nyingi kuashiria idadi ya wanyama aliowaua.

8. Sifa ya ubora wa kitu au jambo lolote.

Mfano: Kutoga masikio ni alama ya utamaduni wa baadhi ya makabila ya Kiafrika.

9. Kiashiria kama vile kituo kikuu, mkato, mabano, parandesi, nukta pacha au nukta mkato, kinachotumika katika uakifishaji.

Katika lugha ya Kiarabu, neno alama limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu alaamah( soma: alaamatun/alaamatan/alaamatin علامة), nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo:

1. Dokezo, ishara, athari.

2. Mpaka unaogawa maeneo mawili ya ardhi.

3. Kitu kinachoweka njiani kwa ajili ya kuwaelekeza watu eneo au kitu fulani.

4. Asilimia ya maksi anazotoa mwalimu kwa mwanafunzi kuhusu kiwango cha maarifa au tabia za mwanafunzi husika.

Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu  alaamatun  علامة lilipoingia katika Kiswahili  na kutoholewa kuwa neno alama lilichukua baadhi ya maana katika lugha asili - Kiarabu na kuacha maana nyingine.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)