MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'TAJIRIBA/TAJRIBA'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'TAJIRIBA/TAJRIBA'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'TAJIRIBA/TAJRIBA'

Neno *tajiriba/tajriba* katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* yenye maana zifuatazo:

1. Ujuzi na maarifa aliyonayo mtu kutokana na kufanya kazi au kuishi kwa muda mrefu.

2. Ujuzi au maarifa aliyonayo mtu kuhusu maisha kwa ujumla kama matokeo ya kufanya jambo mara nyingi au kuishi kwa muda mrefu.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *tajiriba/tajriba*( *soma: tajribatun/tajribatan/tajribatin تجربة)*  ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo:

1. Jaribio linalofanywa kwa kitu fulani na kwa umakini ili kupata matokeo fulani au kuthibitisha uwepo wa kitu fulani.

2. Kinachotangulia kufanywa ili kubaini kasoro katika kitu fulani na kuisahihisha au kuirekebisha.

3. Jaribio la mchezo wa kuigiza.

4. Uzoefu unaotokana na ujuzi au maarifa aliyonayo mtu kutokana na kufanya kazi au kuishi kwa muda mrefu.

5. Jaribio la Kisayansi.

Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu *tajribatun/tajribatan/tajribatin تجربة)*  lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa  *tajiriba/tajriba* maana yake katika lugha ya asili - Kiarabu haikubadilika.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)