MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'MUKAFAA'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'MUKAFAA'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'MUKAFAA'

Neno *mukafaa* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino [Ngeli: u-/i- wingi: mikafaa]*  yenye maana ya fedha ya ziada mbali na mshahara anayolipwa mfanyakazi kutokana na faida iliyopatikana au kwa kuvuka lengo.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *mukafaa*( *soma: mukaafa-atun/mukaafa-atan/mukaafa-atin مكافاة )*  ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo:

1. Tendo-jina *masw-dar مصدر* linalotokana na kitenzi cha Kiarabu *kaafa-a كافأ* chenye maana ya: (1) kumpa mtu tuzo baada ya kufanya vizuri katika jambo fulani. (2) kulinganisha kazi mbili. (3) amejilingajisha na mwengine na kuwa sawa naye.

2.  Kumtendea mtu wema kama alivyokutendea.

3. Kitu chenye hadhi na heshima kubwa anachopewa mtu kama zawadi baada ya kufanya vizuri katika jambo fulani; *tuzo* .

Kinachodhihiri ni kuwa neno *mukaafa-atun/mukaafa-atan/mukaafa-atin مكافاة* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *mukafaa* maana yake katika lugha ya asili - Kiarabu haikubadilika.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)