MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'AJUZA'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'AJUZA'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AJUZA'

Neno ajuza katika lugha ya Kiswahili ni nomino [Ngeli: a-/wa- wingi: maajuzi]  yenye maana mtu wa jinsi ya kike aliyezeeka sana; mwanamke aliyekonga sana.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili ajuza( soma: ajuuzatun/ajuuzatan/ajuuzatin عجوزة )  limetamatishwa na herufi ya Kiarabu taau (t ة) ya mkunjo ambayo ni alama ya jina la kike ingawa katika lugha ya Kiarabu neno hili hutumika bila ya hiyo herufi (t ة) yaani: ajuuzun/ajuuzan/ajuuzin  عجوز kwa mwanamume na mwanamke.

Neno hili linatokana na kitenzi cha Kiarabu ajaza عجز  chenye maana: ameshindwa.

Neno ajuuzun (soma: ajuuzun/ajuuzan/ajuuzin  عجوز ) katika lugha ya Kiarabu lina maana zifuatazo:

1. Mtu wa jinsi ya kike au kiume aliyezeeka. Huitwa pia harimu هرم .

2. Siku za baridi kali ayyaamul ajuuzi أيام العجوز katika msimu wa baridi ambazo ni siku saba: siku nne za mwisho wa mwezi Februari na siku tatu za mwanzo wa mwezi Machi .

3. Pombe.

4. Ardhi.

5. Simba

6. Mbwa mwitu.

7. Sungura.

8 . Ng'ombe jike.

9 . Ngamia jike.

10 . Sindano.

11 . Kisima.

12 . Bahari.

13 . Shujaa

14 . Mfanyabiashara.

Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu ajuuzun/ajuuzan/ajuuzin عجوز llilipoingia katika  Kiswahili na kutoholewa kuwa neno ajuza  Waswahili walichukua maana moja tu ya mtu aliyekonga na wakamhusisha mtu wa jinsi ya kike tu na kumuacha mtu wa jinsi ya kiume kama walivyoziacha maana nyingine 13 za neno hili katika lugha ya Kiarabu.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)