MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA MANENO 'BABU' NA 'ABUWABU'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA MANENO 'BABU' NA 'ABUWABU'
#1
*TANBIHI: KWA KUTEKELEZA USHAURI WA WADAU WA MAKALA HAYA YA ETIMOLOJIA WALIOTAKA KUORODHESHWA MAANA ZOTE ZA NENO BABU KATIKA KISWAHILI, KWA UNYENYEKEVU MKUBWA TUMETEKELEZA HILO*

*HII NDIYO ETIMOLOJIA YA MANENO 'BABU' NA 'ABUWABU'.*

Neno *babu* katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo:

1. *Nomino: [Ngeli: a-/wa- , wingi: mababu]* i) baba mzazi wa baba au mama, ii) mzee mwanamume, iii) msimbo au jina la kujipangia wanalojiita wanawake kwenye shughuli au mikusanyiko yao.

2. *Nomino: [Ngeli: a-/wa-]* mshauri au kiongozi wa kiume katika chama au kikundi cha wanawake.

3. Maradhi ya kukakamaa mwili mzima na kupoteza fahamu yanayowashambulia watoto wadogo; degedege.

4. *Nomino: [Ngeli: i-/zi-]* kipimo au kiwango maalumu cha kitu aghalabu kitambaa cha nguo.

5. *Nomino: [Ngeli: i-/zi-]* mahali pa kuingilia katika jengo; mlango.

6. *Nomino: [Ngeli: i-/zi-]* sehemu ya kitabu, onyesho, sura, wajihi, juzuu.

Katika lugha ya Kiarabu, neno *babu* ni nomino ya Kiarabu  *baabun/baaban/baabin باب* yenye maana zifuatazo:

1. Sehemu ya kuingilia katika jengo, nyumba, chumba na mfano wake.

2.  Kitu kinachoziba sehemu ya kuingilia au kutokea katika jengo, nyumba, chumba na mfano wake na kinachotengenezwa kutokana na mbao, chuma na kadhalika.

3. Sehemu ya kitabu inayozungumzia maudhui fulani; *faslu* .

Neno *abuwabu* katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo:

1. *Nomino: [Ngeli: i-/zi-, wingi: ziabuwabu]* fremu zenye mifuniko zilizopachikwa kwenye sehemu za wazi katika jengo na zilizotengwa kwa ajili ya kuingilia au kutokea.

2. *Nomino: [Ngeli: i-/zi-, wingi: ziabuwabu]* nafasi katika ukuta wa jengo inayoweza kufungwa au kufunguliwa kuruhusu kutoka au kuingia.

3. Milango (kishairi).

Katika lugha ya Kiarabu, neno *abuwabu* (soma: *ab-waabun/ab-waaban/ab-waabin ابواب* ) ni nomino iliyo wingi wa neno la Kiarabu *baabun/baaban/baabin  باب* tulilolifafanua hapo juu.

Kinachodhihiri ni kuwa Waswahili wamelichukua neno *babu* (soma: *baabun/baaban/baabin باب* )  wakalipa maana ya *mlango na sura katika kitabu*  na wakalichukua neno *abuwabu* ambalo ni wingi wa neno la Kiarabu *baabun باب* wakalipa maana ya *mlango* na Kamusi ya Kiswahili Sanifu (TUKI/1981) ikasajili maana ile ya lugha ya asili - Kiarabu, *milango* lakini ikaipambanua kuwa ni maana ya kishairi.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)