MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI: JOYA

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
SHAIRI: JOYA
#1
>>> JOYA  <<<<.
Nazi niliyonunua, nimekuta joya ndani.
Ndipo nikafurahia, kuila kwa umakini.
Baada kujibwagia,ladha yake sitamani
Joya lina ladha gani, malenga niambiyeni ?

Ukitazama kwa macho, nyeupe nyama laini.
Huliwa kwake kificho, mja hali hadharani.
Malenga ni chambilicho, majoya hayalingani.
Joya lina ladha gani, malenga niambiyeni?

Wapendayo husifia, raha iko utosini.
Wao wanapojilia, husema tamu ayuni.
Kwangu naona fadhaa, kulila  silitamani.
Joya lina ladha gani, malenga niyambiyeni.

Hebu nasi tuambie, utamu wa joya nini.
Nazi tena ninunue, nile joya ukumbini.
Nambie nami nijue, isiwe ni kutuhini.
Joya lina ladha gani, malenga tuambiyeni?

Beti zangu nii haba, nakomea kituoni.
Akina mama na baba, joya lina kitu gani.
Wengj hula wakishiba, joya lina siri gani.
Joya lina siri gani, na ladha tuambiyeni.

WAHENGA NAOMBENI JIBU
AMOUR

joya

NOMINO
  • 1
    nyama nyororo nyeupe inayoota ndani ya nazi inapotaka kuota, pengine hujaza kifuu.

    ‘Joya ya nazi’

    ‘Nyororo’

Matamshi
joya
/ʄɔja/

Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)