MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
OSW 234/224 : FASIHI SIMULIZI >>>>MTIHANI WA MWAKA (ODEX) 2016: MAJIBU

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
OSW 234/224 : FASIHI SIMULIZI >>>>MTIHANI WA MWAKA (ODEX) 2016: MAJIBU
#1
OSW 234/224 : FASIHI SIMULIZI >>>>MTIHANI WA MWAKA (ODEX) 2016: MAJIBU 

 1. Kila jamii ina fasihi simulizi yake tofauti na jamii nyingine. Kwa vipi?

MAJIBU

Ni kweli kila jamii ina fasihi simulizi yake tofauti na jamii nyingine. Utofauti huo unatokana na mambo mbalimbali kama vile:

- Mila na desturi

- Mazingira

- Amali

- Historia ya jamii husika

- Misingi ya asili ya jamii husika

Misingi ya jamii ndio msingi wa fasihi ya jamii husika na utofauti wa misingi hiyo ya kila jamii hufanya kila jamii iwe na fasihi simulizi yake.

 2. “Fasihi simulizi iko Afrika tu! Ulaya hakuna fasihi simulizi!” Jadili kauli hii.

MAJIBU

Jamii za ulaya haziamini juu ya kuwepo kwa fasihi simulizi, wao wanaamini kuwa maandishi “Litera” ndiyo fasihi pekee. Fasihi za Kiafrika huchukuliwa kuwa ni ushenzi (kutostaarabika) na ushamba. Fasihi simulizi ya Afrika kwa asili haiwekwi katika maandishi kutokana na uwasilishwaji wake na umuhimu wake. Miongoni mwa fasihi simulizi za Afrika ni:

Jando na Unyago, haya ni mafundisho ambayo hutolewa kwa vijana wa kiume na wa kike mtawalia. Mafundisho haya humjenga kijana wa kiafrika kuwa mchapakazi, muadilifu na mtetezi wa jamii yake.

Matambiko, ni ibada zinazowapa waafrika fursa ya kuwasiliana na Mungu wao na kuelezea mahitaji yao ili kupata ufumbuzi. Matambiko husaidia jamii kudumisha umoja na mshikamano na kutatua changamoto zao za kiimani. Jamii za ulaya huona matambiko kuwa ni dhambi.

Ngoma, ni fasihi simulizi ya kiafrika ambayo hutumiwa kuburudisha, kuelimisha na kuleta jamii pamoja katika matukio mbalimbali ya kijamii yafuraha au huzuni. Kila jamii huwa na ngoma yake na hutambulishwa kwa hiyo.

Hadithi za kimapokeo, hutumiwa kupitishia maarifa ya kijamii kwa vizazi vijavyo kupitia masimulizi ya mambo hayo kwa vijana na watoto. Hadithi kama ngano, vigano, tarihi na visasili hubeba amali mbalimbali za jamii.

Miviga, ni fasihi simulizi ya kiafrika ambayo hufanyika msimu wa mavuno na huambatana na sherehe za kijamii kama kusimika viongozi, kumtoa mwari au kuwapeleka vijana jandoni. Miviga hutumiwa pia kuwaleta watu pamoja na kuwasahaulisha watu madhila mbalimbali yanayowakabili.

Kwa ujumla fasihi simulizi inapatikana Afrika kwa kiasi kikubwa kutokana na mazingira na mahitaji ya jamii husika.

 3. “Wa mbili havai moja na maskini akipata matako hulia mbwata.” Eleza maana na  dhima ya semi hizi.

MAJIBU

Katika maisha kila mtu amepangiwa bahati yake. Kuna ambao kupata ni kawaida na kuna wale ambao kupata sio kawaida. Makundi haya mawili ya watu yanazaa methali mbili ambazo ni “Wa mbili havai moja” na “Maskini akipata matako hulia mbwata.” Methali hizi zinafafanuliwa kama ifuatavyo:

Wa mbili havai moja, methali hii inamaana kuwa alichopangiwa mtu na mola ndicho atakachopokea hata kama patatokea watu wenye chuki na husuda dhidi yake. Kuna watu huwa hawafurahishwi na mafanikio ya watu wengine kiasi cha kufanya mipango ya kukwamisha mafanikio ya mtu mwingine.

Dhima ya methali hii ni kuwahamasisha watu kuongeza bidii katika kutafuta mafanikio yao badala ya kuhangaika kuzuia mafanikio yaw engine ambayo hasa ni mipango ya Mungu.

Maskini akipata matako hulia mbwata, methali hii inaelezea tabia ya baadhi ya watu kuonesha ufahari na kujitapa pindi wanapopata mafanikio kidogo maishani mwao. Watu hawa hasa ni wale ambao hawaamini kama wanastahili kufanikiwa ndio maana wakipata kila mtu atajua na wanaona fahari.

Dhima ya methali hii ni kuwatahadharisha watu kutoonesha ufahari wanapofanikiwa kwa kujua kuwa mafanikio huweza kuwa ya muda nay a kupita lakini utu na uhusiano mwema hudumu daima.

Kwa ujumla methali ni kipengele muhimu cha semi chenye kuhifadhi na kurithisha hekima na busara za jamii.

 4. Fasihi simulizi huchapuza kazi. Mfano: Kilimo n.k! Thibitisha dai hili.

MAJIBU

Chapuzo ni fasihi simulizi itumiwayo sana kuchochea na kuhimiza kazi katika jamii. Nyimbo za kuchapuza hutofautiana kulingana na kazi husika, kwa mfano.

Chapuzo za wakulima, hizi huitwa wawe na huimbwa wakati watu wakiwa shambani. Wawe huimbwa kufuatana na mapigo ya zana, mathalan kupanda na kushuka kwa jembe wakati wa kulima. Nyimbo hizi ni maarufu sana kwa jamii ya wasukuma.

Chapuzo za wavuvi, hizi huimbwa na wavuvi wawapo majini katika shughuli zao hasa usiku. Nyimbo hizi huitwa kimai. Hutumika kuwaondolea wavuvi ukiwa na unyonge.

Nyimbo za vita, hizi huimbwa na wanajeshi msimu wa vita ili kuwapa morali wanajeshi wawapo vitani. Chapuzo huwafanya wanajeshi wasiwaze sana kuhusu madhara ya vita na kujiondolea woga na hofu ya kufa.

Kwa ujumla kazi yoyote huwa nyepesi sana iwapo itaambatana na chapuzo kama kiburudisho cha mfanyaji kazi hiyo.
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)