MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
USHAIRI: UTAMU WA KISWAHILI

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
USHAIRI: UTAMU WA KISWAHILI
#1
UTAMU WA KISWAHILI
Kanda ndipo uingiye, mganga akutibiye,
Kanda kinyunya kijaye, andazi tulibugiye,
Kanda sio mwaminiye, vitu vyako ajiliye,
Kanda ijaze ijaye, waikute na wajaye,
Kanda ulishikiliye, na ndipo uogeleye.

Koto towa kwa alimu, mwanao akasomeya,
Koto atiwe nidhamu, waja kuwaheshimiya,
Koto hunasa adimu, papa walojifichiya,
Koto inakulazimu, kazi ukajifanyia,
Koto mizizi muhimu, tumbole tuktibiya.

Ota mmea ukue, hima tuupaliliye,
Ota ndoto irudie, kesho utusimuliye,
Ota moto ukukae, ukizi uunguye,
Ota pindo jipindiya, ukishajikaukiye,
Ota nini kitokee, mkono nifumbatie.

Paa samaki paruza, maganda yasibakiee,
Paa angani paliza, hukohuko upotee,
Paa muue kiweza, kitoweo tutowee,
Paa usije egeza, upepo ukaanue,
Paa moto kupaliza, mote kajikolezee.

Kata vipande vigawe, nusu nusu tupatie,
Kata maji ichotiwe, kisima tuinamie,
Kata isitawaliwe, kwa mabavu tukimbie,
Kata iache sitowe, damu isijivujie,
Kata kichwa situwe, mzigo ujitwikie.

Chenga hima avuliwe, sokoni anunuliwe,
Chenga mtu akimiwe, omba mola asijuwe,
Chenga vipande vigawe, tugawane mimi nawe,
Chenga weka uchambuwe, mchele tujipikiwe,
Chenga mpira siliwe, ndugu yako akimbiwe.

Susa jambo usitende, zira na utokomee,
Susa tikisa mtende, watu usidondokee,
Susa toa asigande, mwilini akuzoee,
Susa si tamu kipande, mua nisisogelee,
Susa huleta udende, mswaki jisugulie.

Futa kilichochomekwa, kisu kiweke pembeni,
Futa maji kukaukwa, na maji tukalieni,
Futa kuta kudondokwa, tukabaki gharikani,
Futa jambo kufanyikwa, umsusie jirani,
Futa bora kumwepuka, anayosumu kinywani.

Fumba kinywa sitamke, ukimya ukujiliye,
Fumba mja sijulike, mwachie akafumbuye,
Fumba viriga ushike, kiganja ujijaziye,
Fumba chini uoneke, unyayo tuutambuye,
Fumba suka usukike, maiti tukazikiye.

Funga lango siingiye, mwivi aje akwibiye,
Funga goli liingiye, ushindi tushangiliye,
Funga uyadhamiliye, mambo yako jitendeye,
Funga kula jizuiye, saumu uvumiliye,
Funga uiheshimiye, dhambi usiangukiye.

Chungu ladha hupoteya, hufanana na shubiri,
Chungu ukikipikiya, wongeza tamu futari,
Chungu muwa hudoweya, kuitafuta futari,
Chungu ikikutokeya, uzuri utaghairi,
Chungu mali kijaziya, tajioneya fahari.

Bao goli la kandanda, waja tukashangiliya,
Bao mchezo kuunda, kucheza tafurahiya,
Bao ubao ‘so ganda, nyumba tukaezekeya,
Bao mganga hupenda, ramuli kujifanyiya,
Bao wanaokuwinda, huachi kujioneya.

Pasi na kunijulisha, akaja kunigongeya,
Pasi nguo kikausha, na moto ukikoleya,
Pasi mpira kuvusha, jirani kumpigiya,
Pasi vidato kupisha, masomo kuendeleya,
Pasi piga na safisha, nchi nje jiendeya.


Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 2 Guest(s)