MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA MANENO ' ADALA', 'ADILI' NA 'UADILIFU'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA MANENO ' ADALA', 'ADILI' NA 'UADILIFU'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA MANENO ' ADALA', 'ADILI'  NA 'UADILIFU'.

Neno adala katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo:

1. Nomino : Mwenendo wa kutenda haki bila ya kupendelea upande wowote; uadilifu .

2. Nomino: Umoja wa kundi au jamii pana wa kujihusisha kikamilifu na shughuli za kundi hilo.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili adala (soma: adaalatun/adaalatan/adaalatin عدالة ) lina maana zifuatazo:

1. Nomino : Mambo manne bora yaliyokuwa mihimili ya wanafalsafa wa kale: Hekima, Ushujaa, Ucha-Mungu (Usafi wa moyo) na Adala (Uadilifu).

2. Nomino : Tendo - jina la kitenzi cha Kiarabu adala عدل  chenye maana ya 'amefanya insafu/adala/uadilifu.

Neno adili katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo:

1. Nomino : Hali ya kuwa na uelekevu wa moyo; …
[6:42 AM, 12/24/2021] +255 713 603 050: HII NDIYO ETIMOLOJIA YA MANENO ' ADALA', 'ADILI'  NA 'UADILIFU'.

Neno adala katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo:

1. Nomino : Mwenendo wa kutenda haki bila ya kupendelea upande wowote; uadilifu .

2. Nomino: Umoja wa kundi au jamii pana wa kujihusisha kikamilifu na shughuli za kundi hilo.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili adala (soma: adaalatun/adaalatan/adaalatin عدالة ) lina maana zifuatazo:

1. Nomino : Mambo manne bora yaliyokuwa mihimili ya wanafalsafa wa kale: Hekima, Ushujaa, Ucha-Mungu (Usafi wa moyo) na Adala (Uadilifu).

2. Nomino : Tendo - jina la kitenzi cha Kiarabu adala عدل  chenye maana ya 'amefanya insafu/adala/uadilifu.

Neno adili katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo:

1. Nomino : Hali ya kuwa na uelekevu wa moyo; unyoofu.

2. Kitenzi si elekezi: adil.i fanya haki au wema bila ya upendeleo.

3. Kivumishi: -enye haki, -siopendelea.

4. Nomino : Hali ya watu kuishi kwa usawa bila  kubaguana.

5. Nomino : Utaratibu wa maisha unaozingatia  sheria na kanuni zilizowekwa na jamii husika.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili adili (soma: adlun/adlan/adlin عدل ) lina maana zifuatazo:

1. Nomino : Kumpa mtu haki yake na kumnyang'anya kisicho haki yake; insafu .

2. Nomino : Mwenza wa mtu.

3. Nomino: Fidia.

4. Nomino : Malipo, Jazaa.

Ama neno ' uadilifu ' limetoholewa kutoka neno 'adili' na kupewa maana ya mwenendo wa kutenda haki bila ya kupendelea upande wowote.

Neno hili, kwa maweko yake, si neno la Kiarabu.

Kinachodhihiri ni kuwa maneno adala (soma: adaalatun/adaalatan/adaalatin عدالة) na adili (soma: adlun/adlan/adlin عدل) yalipoingia katika lugha ya Kiswahili na kutoholewa kuwa maneno adala na adili maana zake za msingi katika Kiarabu hazikubadilika.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)