MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SABABU ZA ATHARI ZA KIMATAMSHI

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
SABABU ZA ATHARI ZA KIMATAMSHI
#1
Matamshi ya maneno katika lugha ya Kiswahili huathiriwa au hukosewa kutokana na sababu zifuatazo:
1. Athari za lugha ya kwanza/lugha mama, kwa mfano:
  • hachezagi badala ya huwa hachezi……………..Msukuma
  • karamu badala ya kalamu………………………..Mkurya
  • Dhawadi badala ya zawadi………………………Mzaramo/Mgogo
  • Ntoto badala ya mtoto……………………………Mmakonde
  • Fiatu fyangu badala ya viatu vyangu………..Mnyakyusa
  • Thithi thote badala ya sisi sote…………………Mpare
2. Kutokuwa na elimu
Mtu akikosa elimu au ufahamu wa kutosha kuhusu lugha fulani inaweza kusababisha kukosea matamshi ya maneno ya lugha husika.
3. Athari za lugha za kigeni
Mtu anapozungumza lugha za kigeni mara kwa mara katika mawasiliano yake humfanya awe na uzoefu na lugha husika. Hivyo, wakati anapozungumza lugha yake (lugha mama) hujikuta akiathiriwa kimatamshi na kimsamiati.
4. Mazoea
Wakati fulani mazoea ya mtu katika lugha yake humfanya aathiriwe katika vipengele fulani vya lugha anapozungumza lugha nyingine au na mtu mwingine akidhani ataeleweka. kwa mfano, zalau badala ya dharau, na zambi badala ya dhambi.
5. Athari za kimaumbile
Mtu anapokuwa na tatizo kwenye ala za sauti, hususan kuwa na kithembe, huweza kuathiri matamshi ya lugha sanifu. Kwa mfano, thalamu badala ya salamu.
6. Kasumba za wasomi
Mara nyingi wasomi wengi hupenda kuzungumza lugha za kigeni, ikiwemo Kiingereza, wakati wa mazungumzo yao wakiamini kuwa kwa kufanya hivyo kutadhihirisha elimu au usomi wao mbele ya wengine.
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)