MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'ABUWABU'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'ABUWABU'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO  ' ABUWABU'

Neno *abuwabu* katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo:

1. Nafasi katika ukuta wa jengo inayoweza kufungwa na kufunguliwa kuruhusu kuingia au kutoka; mlango.

2. Fremu zenye mifuniko zilizopachikwa kwenye sehemu wazi katika jengo  na zilizotengwa kwa ajili ya kuingia na kutokea.

3. Milango (Kamusi Teule ya Kiswahili (EAEP), Toleo la Kwanza, 2014, Ukurasa wa 2.)

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *abuwabu* ( soma: *abuwaabun/abuwaaban/abuwaabin* *ابواب* ) ni nomino ya Kiarabu ikiwa ni wingi wa neno baabun/baaban/baabin باب lenye maana zifuatazo:

1. Sehemu ya kuingilia kwenye jengo, nyumba au chumba na mfano wake.

2. Kinachoziba sehemu ya kuingilia katika jengo, nyumba au chumba na mfano wake, kinachotengenezwa kutokana na mbao au chuma  na mfano wake.

3. Sehemu ya maandishi ya Kitabu yaliwekewa anuani maalumu; sura (katika kitabu).

4. Eneo la kazi au taaluma haadhaa baabuhu hili ni eneo lake la kazi/taaluma.

Kinachodhihiri ni kuwa katika Kiswahili (Kamusi Kuu ya Kiswahili na Kamusi ya Kiswahili ya Karne ya 21) kumechukuliwa neno lililo katika wingi *abuwabu* ( *abuwaabun ابواب* ) lenye maana ya *milango* na likapewa maana ya neno la Kiarabu lililo katika umoja  *baabun* *باب* *(mlango)* ingawa Kamusi ya Kiswahili Sanifu (TUKI - TOLEO LA 3 - UKURASA WA 24) mbali ya kulisajili neno *babu* kama neno lenye asili ya Kibantu lenye maana anuai, imelisajili pia kama neno (nomino) lenye asili ya Kiarabu likiwa na maana ya:
1. Aina ya kipimo cha kitambaa: ~ pana kitambaa kipana; ~ ndogo kitambaa chenye upana mdogo; ~ kubwa kitambaa chenye upana mkubwa.

2. Neno (nomino) la kishairi ya: sura ya kitabu au buku; mlango.

Hata hivyo, katika Kamusi Teule ya Kiswahili (EAEP) na Kamusi ya Kiswahili - Kiingereza (TUKI) neno hili limesajiliwa kwa maana ileile ya milango, wingi wa neno *baabun* (mlango).

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)