12-03-2021, 06:35 AM
Kitenzi kishirikishi
Mifano
- Yeye ‘ndiye mwalimu wao
- Sisi tu wanafunzi watiifu
- Jembe li shambani
Kitenzi kishirikishi (alama yake ya kiisimu ni: t) ni kitenzi ambacho hujulisha hali ya kuwepo au kutokuwepo kwa uhusiano/ushirikiano baina ya vipashio vya lugha. Uhusiano huo unaweza kuwa katika tabia, hali, au mazingirafulani.
Uchambuzi
- Khadija ni mwizi (ni, ni hali ya kuyakinisha ya kwamba Khadija ana uhusiano na tabia ya wizi).
- Joseph alikuwa mwalimu wetu (tendo kamilifu).
- Amina hakuwa mchoyo (hapa inakanusha ya kwamba Amina hana uhusiano tabia ya uchoyo).
- Kikombe ki mezani (hapa kipashio cha ki kimetumika kutaja mazingira au mahali kikombe kilipo – kiko mezani).
- Juma yu mgonjwa (hapa inataja tena hali ya nafsi – ni mgonjwa).
Angalizo: Kitenzi kishiriki alama yake ni t ndogo.
Aina za vitenzi vishirikishi
Aina za vitenzi vishirikishi vimegawanyika katika makundi makuu mawili – navyo ni:
Mwl Maeda