MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

KIDATO CHA TATU: NGELI ZA NOMINO

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
KIDATO CHA TATU: NGELI ZA NOMINO
#1
Kuzielewa  Ngeli
Upatanishi wa Kisarufi katika Sentensi
Fafanua upatanishi wa kisarufi katika sentensi
Ngeli ni vikundi vya majina ya Kiswahili. Ngeli za nomino ni utaratibu unaotumika kuweka nomino katika matabaka au makundi yanayofanana.
Mfano
Mfano:
  1. Maji yakimwagika hayazoleki
  2. Mayai yaliyooza yananuka sana
  3. Yai lililooza linanuka sana
  4. Maji liliomwagika halizoleki
Katika mifano hii tunaona kwamba sentensi a, b na c ziko sahihi wakati sentensi d sio sahihi, hii ni kwa sababu imekiuka upatanisho wa kisarufi. Kwa maana hiyo sentensi ‘a’ ipo katika ngeli ya YA-YA na senthensi b na c zipo katika ngeli ya LI-YA. Sentesi d sio sahihi kwa sababu nomino maji haina wingi, kwa hiyo haiwezi kuingia katika ngeli ya LI-YA. Kwa msingi huu ngeli za nomino huzingatia sana upatanisho wa kisarufi.
Jedwali lifuatalo linaonesha ngeli za nomino kwa misingi ya upatanisho wa kisarufi.
[Image: SAM_2.JPG][url=https://3.bp.blogspot.com/-FwMTwYT3gqA/WgU5KXhuZnI/AAAAAAAACoU/hBwqq1qpXzcqzlsHfpokb1LRgTayW9EEQCLcBGAs/s1600/SAM_2.JPG]
Baadhi ya matumizi ya ngeli ni pamoja na haya yafuatayo:
  • Hutumika kupanga majina ya lugha katika makundi yaliyoshikamana na kutofungamana kutokana na kigezo muhimu.
  • Hutumika kutambulisha maumbo ya umoja na wingi katika majina na vivumishi.
  • Hutumika katika upatanishi wa kisarufi katika sentensi.
  • Hutumika katika kuonyesha uhusiano uliopo baina ya lugha za Kiswahili na lugha zingine.
  ZOEZI  
Upatanisho wa kisarufi uliofanyika katika sentensi hii “Yai limeoza”
unahusiana na ngeli gani?
A
A-WA
B
I-ZI
C
LI-YA
D
KI-VI
Upatanishi wa kisarufi katika sentensi hutawaliwa na ___
A
Kivumishi
B
Kitenzi
C
Kiunganishi
D
Jina
‘Gari yameuzwa’ ili kuleta upatanishi wa kisarufi ni kiambishi gani cha
 ngeli kinafaa kiwekwe kwenye neno yameuzwa badala ya kiambishi {ya-}?
A
A-
B
Ki-
C
Li-
D
U-
Viambishi vya upatanishi wa kisarufi katika sentensi hukaa ___ mwa neno husika.
A
Katikati
B
Mwanzoni
C
Mwishoni na katikati
D
Mwishoni
Upatanishi wa kisarufi katika sentensi hujitokeza kati ya nomino au
viwakilishi vyake na___
A
Vitenzi
B
Vivumishi
C
Viunganishi
D
Vielezi
Habari zenye Upatanishi wa Kisarufi
Andika habari zenye upatanishi wa kisarufi
Baadhi ya matumizi ya ngeli ni pamoja na haya yafuatayo:
  • Hutumika kupanga majina ya lugha katika makundi yaliyoshikamana na kutofungamana kutokana na kigezo muhimu.
  • Hutumika kutambulisha maumbo ya umoja na wingi katika majina na vivumishi.
  • Hutumika katika upatanishi wa kisarufi katika sentensi.
  • Hutumika katika kuonyesha uhusiano uliopo baina ya lugha za Kiswahili na lugha zingine.
 ZOEZI 
Tambua kosa la upatanishi wa kisarufi katika sentensi hii “kuta
 imebomoka jana asubuhi,”
A
Kuta
B
Kuta imebomoka
C
jana asubuhi
D
Asubuhi
Onesha kosa la upatanishi wa kisarufi katika sentensi hii ‘John
wamenunuliwa kiatu kizuri.’
A
John wamenunuliwa
B
Kiatu kizuri
C
Kiatu
D
Kizuri
‘Watu iko mingi’ katika sentensi hiyo kuna ukiukaji wa kanuni za___
A
Miundo
B
Viambishi
C
Maneno
D
Upatanishi wa kisarufi
Ipi kati ya sentensi zifuatazo haina upatanishi sahihi wa kisarufi?
A
Mauti hizi zinanuka.
B
Maiti zile zinanuka.
C
Maiti huyu ananuka.
D
Maiti hii inanuka.
Ipi kati ya sentensi zifuatazo ina tatizo la upatanishi wa kisarufi?
A
Mtoto anakula.
B
Watoto anakula.
C
Watoto anakula.
D
Mtoto anakula.
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)