MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MALENGO YA ISIMU

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
MALENGO YA ISIMU
#1
Malengo ya Isimu
ISIMU basi, ni taaluma ambayo inachunguza na kuweka wazi kanuni hizi ambazo ndio msingi wa kila lugha. Hivyo lengo kuu na la kwanza la taaluma ya isimu ni kuchambua na kuelezea maarifa aliyo nayo mjua lugha kuhusu lugha yake. Di kufanya hivyo, mwanaisimu anachunguza lugha tofauti na kuona taratibu zinazotawala sarufi za lugha bizi, na kutokana na taratibu hizo anatoa majumlisho kuhusu lugha za wanadamu kwa jumla. Kwa maneno mengine, mwanaisimu anacbofanya ni kutafiti undani wa sarufi-jumla kutokana na uchambuzi wake wa sarufi-maalumu tofauti (yaani sarufi za lugba mbalimbali). Majina ya vipashio ambavyo tunavijua katika masomo ya sarufi, kama vile neno, sentensi, nomino, vitenzi, n.k., ni sehemu ya sarufi-jumla. Hivi ni baadhi ya vipashio ambavyo, kutokana na ucbambuzi wa lugha tofauti, vimegundulika kuwepo katika lugha nyingi za wanadamu zilizokwisha tafitiwa. Lakini mbali na ujumla wa vipashio hivi, maswali mengine kama ‘neno lina muundo gani’ ni lazima yajibiwe tofauti kwa kila lugha. Ni maswali ambayo yanahusu sarufi-maalumu. Kwa mfano, sifa moja ya nomino katika Kiswahili ni kuwa na vipashio vinavyoonyesha umoja na vile vinavyoonyesha wingi (mti:miti; kiti:viti); ambapo katika Kiingereza bakuna kipashio maalumu cha umoja, bali kipo cha wingi (tree:trees; chair:chairs).
Ni muhimu kusisitiza kuwa lengo la isimu si kuwafundisha watu jinsi ya kuzungumza lugha yao, yaani kipi waseme na kipi waache. Iliposemwa hapo juu kuwa isimu inaweka wazi kanuni zinazotawala lugha, ambazo wazungumzaji wanazitumia bila wao wenyewe kuzijua, haikuwa na maana kuwa sasa mwanaisimu aanze kuwawekea wazungumzaji sheria za jinsi ya kutumia lugha yao. Mtu akishakuwa na maarifa juu ya kitu fulani, anaweza kuyatumia kwa njia yoyote anayotaka, vizuri au vibaya. Maarifa ya lugha halikadhalika. Lengo la isimu si kuwaasa wazungumzaji wasiseme bivi au vile, bali ni kuyafafanua na kuyaeleza kwa ustadi yale wanayoyafanya. Mwanaisimu anachambua lugha yeyote ile bila kujali inazungumzwa wapi, au na nani, au kwa madhumuni gani. Ikishakubalika kuwa X ni lugha, basi ina maana kuwa inatii sifa zote zinazohusu lugha, na hivyo ni haki kuichunguza, hata ikiwa kwa mazoea yetu ya kibinadamu, tunaona kuwa wanaozungumza lugha hiyo, au aina hiyo ya lugha, si maarufu kama kundi lingine la wanadamu wanaozungumza lugha Y.
Hata hivyo, ni vema tukubali kuwa neno ‘sarufi’, kwa mazoea ya vyuoni, ambayo ni ya’siku nyingi, limetumika kwa maana finyu zaidi ya hiyo iliyotolewahapojuu, yaani kama kitabu kinachoweka kanuni kuhusu jinsi ya kuzungumza na kuandika lugha fulani. Vitabu vya namna hiyo hasa vimetumika katika kuwafundisha wageni wasiojua lugha fulani, kama kuwafundisha watu Kiswahili ambao wanajua Kiingereza, au kuwafundisha Kiingereza watu ambao wanajua Kiswahili. Baadhi ya vitabu hivyo pia vimetumika kuwafundisha wanaozungumza lugha fulani ‘lahaja sanifu’ ya lugha yao, na hivyo kuwawekea sheria kuhusu maneno na miundo bora inayotakiwa. Sarufi ya namna hiyo inajulikana kama ‘sarufi-sheria’, yaani inayowawekea wazungumzaji sheria kuhusu kipi waseme na kipi wasiseme.
Lakini ni kweli pia kuwa, sarufi, kama somo la darasani linahistoria ndefu na vitabu vingi vimeandikwa ambavyo vimekuwa na lengo la kuchambua tu lugha fulani, bila kukusudia kumfundisha mtu yeyote kuizungumza. Vitabu vya namna hiyo hasa vinalenga wale wanachuoni ambao ni wenyeji wa lugha hiyo. Vipashio vya sarufi ambavyo tumevitaja hapo juu kama ‘nomino, vitenzi’ vimetokana na sarufi kama hizo. Sarufi za namna hii zinaitwa ‘sarufi-fafanuzi’. Kwa kiasi fulani ‘sarufi’ za namna hii zinakaribiana na lengo la isimu tulilotaja, na mara nyingi zinaandikwa na wataalamu ambao wanashughulika na isimu.
Wakati huo huo, ni lazima kusisitiza kuwa wazungumzaji wa lugha fulani katika jamii yao wanao uhuru wa kuweka ‘viwango’ vya usanifu katika matumizi ya lugha yao. Wanaweza kuamua kuwa.matumizi fulani ni ‘mabaya’ au’mabovu’ na mengine ni ‘mazuri’ zaidi; wakaamua pia kuwa maneno fulani hayaonyeshi adabu, na kwa hiyo kuwaasa watoto wao wasiyatumie, n.k. Si kazi ya mwanaisimu kuingilia kati mijadala kama hiyo. Ikiwa maneno au miundo fulani inatumiwa na wazungumzaji wa kawaida wa lugha husika, kazi yake ni kuichambua bila ubaguzi, na kuchunguza kanuni zinazotawala matumizi hayo.
Lengo la pili la isimu, ambalo linatokana na lile la kwanza, ni kuunda nadharia. Nadharia hizi ni za aina mbili: nadharia ya lugha-jumla, na nadharia ya lugha maalumu. Mambo yote mawili yanaathiriana kwa kiasi kikubwa sana. Tumekwisha sema kuwa mwanaisimu, kwa kuchunguza sarufi za lugha tofauti, anafikia mahitimisho fulani kuhusu muundo wa lugha ya mwanadamu kwa jumla. Matamshi mengi yanayotolewa kuhusu muundo wa lugha fulani, ni sehemu ya nadharia ya lugha hiyo. Kwa mfano tunasema kuwa katika sentensi ya lugha ya Kiswahili kiima cha sentensi hutangulia kiarifu, au kuwa kitenzi cha Kiswahili huandamana na vipashio vingine katika kuunda kifungutenzi. Haya ni matamshi ambayo yanahusu muundo wa Kiswahili, ni sehemu ya nadharia ambayo mwanasarufi anaiunda ili kujumlisha yale aliyoyachunguza kuhusu lugha ya Kiswahili. Lakini tukisema kuwa ‘sentensi ya lugha ina kiima na kiarifu’, tunatoa tamko ambalo linahusu lugha ya mwanadamu kwajumla, na hili ni sehemu ya nadharia ya lugha-jumla, ambalo mwanaisimu amelifikia kwa kulinganisha nadharia za lugha tofauti.
Lengo la tatu la isimu ni kuweka wazi mbinu za kuchambua lugha na kutoa hoja za ‘kisayansi’. Zipo sifa kuu tatu za uchambuzi wowote wa kisayansi:
Quote:
(i) uhakikifu: Katika kuzingatia sifa hii, mwanasayansi anapaswa kuhakikisha kuwa yale anayoyasema, pamoja na mahitimisho anayofikia, yanatokana na data zilizo wazi na ambazo zinaweza kuchunguzika. Tamko la kisayansi ni lazima liweze kuthibitishwa na hoja. Umuhimu wa sifa hii ni kuwaasa wanaisimu wasitoe matamko ya juu juu, ambayo hayawezi kuhakikishwa. Katika siku za nyuma taaluma ya uchunguzi wa lugha ilikumbwa na matatizo kama hayo ya kutoa matamko ya jumla kuhusu lugha za wanadamu ambayo yalitokana na fikra za binafsi za wachunguzi. Matamko hayo hayakutegemezwa na hoja zinazoweza kuthibitishwa. Baadhi ya matamko hayo ni yale yaliyodai kuwa kuna lugha ambazo ni bora kimsingi na ziko ambazo ni duni. Hivyo lugha za Ulaya zote zikawekwa katika kundi la kwanza, na lugha za watu ambao sio ‘weupe’ zikawekwa katika kundi la pili. Sababu kubwa ya matamko hayo ilikuwa kwamba watu waliozungumza lugha duni ni watu walio na ustaarabu duni pia, na mara nyingi walitawaliwa na hao waliosemekana kuwa wa utamaduni ulioendelea. Katika kuchunguza lugha za wanadamu, wanaisimu wamethibitisha kuwa hakuna ukweli katika madai kama hayo, ikiwa msingi wa uchambuzi ni kuangalia miundo ya lugha tofauti na sio mahusiano kati ya watu wanaozungumza lugba hizo. Lugha zote za wanadamu zina uchangamano ambao unazifanya ziweze kulinganishwa katika viwango tofauti.
(ii) Ubainifu au uwazi: Hii ni sifa ambayo inawataka wanasayansi kuweka hoja zao wazi bila mzunguko. Ni sifa ambayo inafuatana na hiyo ya hapo juu, na inamtaka mwanaisimu kujiwekea lengo la kupima kwa uangalifu kila analofanya na kuhakikisha kuwa hoja zake anazotoa ili kutegemeza nadharia zake au mahitimisho yake ziko wazi na zinatokana na utafiti wake.
(iii) Upangilifu: Kwa mujibu wa sifa bii, hoja za kisayansi zinapaswa kupangiliwa vizuri. Kwa mfano katika kufafanua muundo wa lugha lazima mwanaisimu aamue ataanza na miundo gani, na kwa mfuatano gani. Uamuzi huu utamsaidia ili asijirudie rudie, na hoja zake ziwe na, mfuatano wa kimantiki. Hoja zisipokuwa na mpangilio unaofaa, zitashindwa pia kutimiza sifa ya uwazi bapo juu, na pia kuweka dosari katika uhakikifu wa hoja hizo.
Tunaweza kuchukua mfano mdogo tu ili kuonyesha jinsi sifa hizi zinavyofanya kazi. Tamko kama “Kiswahili ni lugha ya Kibantu” linapotolewa na mwanaisimu tunategemea kuwa amekwishaeleza, au ana hakika wasikizaji au wasomaji wake wanajua, lugha ya kibantu ina sifa gani, na Kiswahili kinashiriki vipi katika sifa hizo. Ikiwa atatoa tu tamko kama hilo bila taarifa hizo, atakuwa amekiuka sifa ya (i) ya uchambuzi wa kisayansi, na hoja yake pia itakosa uwazi (sifa ya ii). Ikiwa ataendelea kuzungumzia lugha ya Kiswahili na mwishoni kabisa mwa makala yake akazungumzia sifa za lugha za kibantu, atakuwa amekiuka sifa ya (iii) ya upangilifu.
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)