11-27-2021, 08:44 PM
- Kirejeshi kinachopachikwa katikati
Hapa huwa ni O-rejeshi ambayo hupachikwa katikati ya viambishi awali kabla ya mzizi wa kitenzi. Huwa na muundo wa: Awali+rejeshi++mzizi.
Mfano:
- Mtoto aliyekuja jana ameondoka leo
- Kisu kilichopotea ni kizuri sana
- Ugonjwa ulioenea umedhibitiwa sasa
- Nguo iliyochakaa imetupwa
2. O-rejeshi inayopachikwa mwishoni
Hapa huwa na kirejeshi ambacho hupachikwa mwishoni mwa kitenzi. Muundo wake huwa:
Mfano:
- Jino liumalo hung’olewa
- Samba aungurumaye ni mkali
- Msichana apataye mimba hutoa
- Kijana atumwaye amerudi
3. O-rejeshi inayopachikwa kwenye mzizi AMBA
Umbo la AMBA hupachikwa kirejeshi mwishoni na kuwa na muundo wa AMBA+rejeshi. Iwapo mzizi wa AMBA umetumika, kirejeshi huweza kutokea mwishoni mwa mzizi huu na hakiwezi kurudiwa tena katika kitenzi kingine.
Mfano:
- Kitabu ambacho umesoma kimechanika
- Juma amepata adhabu ambayo haiwezi
- Mtoto ambaye atafaulu atapewa zawadi
- Ugonjwa ambao umeenea umedhibitiwa
Kanuni hii isipozingatiwa makosa haya hutokea:
- Kitabu ambacho amechosoma kimepotea
- Kijana ambaye aliyetumwa amerejea
- Wanafunzi ambao watakaojitahidi watafaulu
Mwl Maeda