MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

FIKRA ZA ARISTOTLE KUHUSU UTENDI

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
FIKRA ZA ARISTOTLE KUHUSU UTENDI
#1
Pamoja na kuzungumzia tanzia, Aristotle anajadili juu ya utendi. Anasema kuwa utendi unafanana na tanzia katika sifa zifuatazo:
(i) Kwa upande wa kuzungumzia kadhia moja kuu inayojitosheleza.
(ii) Utendi unaweza kuwa rahisi au mgumu.
(iii) Utendi una mawazo, sehemu ya kati na mwisho.
Tofauti zilizoko kati ya utendi na tanzia ni:
  • Utendi ni mrefu zaidi na kinyume na tanzia hutumia arudhi.

  • Pili, mtunzi ana uhuru na fursa ya kuigiza visa vingi vinavyostaajabisha katika utendi kwa sababu baadhi ya matukio yanayotendeka ni ya kimiujiza.

  • Tanzia mara nyingi huumbwa kutokana na kadhia zinazoweza kutendeka.
Kwa ujumla, maoni ya Aristotle ni muhimu sana katika kuelewa fasihi.
Jambo analolimulikia mwanga Aristotle ni umuhimu wa ploti katika uundaji wa kazi ya Sanaa.
Ploti au msuko ni jinsi hadithi inavyoendelezwa hadi matukio ya mwisho yanapotokea. Wahusika nao ni viumbe wanaotumiwa na mwanasanaa kukuza vitushi vya maigizo yake.
Kwa jumla, fikra za Aristotle zinazorutubisha weledi wa fasihi ni hizi:
(i) Anasema kwamba fasihi si mwigo wa kikasuku. Ni ubunifu unaomwezesha binadamu kumkaribia Mungu.
(ii) Ploti au msuko ni muhimu sana katika ubunifu wa Sanaa.
Jambo hili linaonyeshwa pale ambapo Aristotle anazungumzia tanzia na utendi.
(iii) Aristotle anatuonesha kwamba fasihi itaeleweka vizuri zaidi ikiwa itagawanywa katika tanzu tofauti tofauti.
(iv) Aristotle anasema kwamba fasihi inajitosheleza na inajitawala. Haina haja kutemea taaluma nyingineyo. Haya ni kinyume na Plato, ambaye aliitazama fasihi katika muktadha wa Jamhuri Dhahania.
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)