MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI: JUA LA UTOSI

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
SHAIRI: JUA LA UTOSI
#1
JUA LA UTOSI
Linapochomoza jua,
Asubuhi na mapema,
Sote tunafurahia,
Kulivyokucha salama,
Basi jua husogea,
Mithili mtu kilema,
Katikati hufikia,
Hapo huzua zahama.

Dhahama hapo huzuka,
Jua hugonga utosi,
Wenye afia mashaka,
Kama nzi na mijusi,
Basi hapo hukauka,
Na wengine kwenye nyasi,
mfano mdudu nyoka,
Uhuru kujifilisi.

Lake joto ardhini,
Ni Nani anapekua?
Mwendo huwa mashakani,
Pasi kiatu kuvaa,
Huzidi jasho mwilini,
Mavazi yanavyoloa,
Hali huwa matatani,
Jua huwa lawamani.

Kiu nazo hutubana,
Na maji hatutosheki,
Hata yawe mengi sana,
Au tukanywa wanzuki,
Twataka tena na tena,
Sababu hatutosheki,
Madhila huzidi sana,
Maisha hujaa dhiki.

Jua hapo halikwami,
Lasogea taratibu,
hapo tena halivumi,
Limekwisha tuadhibu,
Tunafunga zetu ndimi,
Muda metupa jawabu,
Tena halitusakami,
Kutuangushia tabu.

Inapofika jioni,
Jua laanzafifia,
Twaanza kulitamani,
Nje tunajitokea,
Tukipata vitamini,
Tena twalifurahia,
Mara jua hatuoni,
Kiza hapo hutokea.

Kiza hapo hutokea,
twaanza kupapasana,
Jua tunalilia,
Livyokwenda mbali sana,
mwishowe tunanyamaa,
Namna hapo hatuna,
Jambo tunaloshangaa,
Kesho tena twaliona.

Ndivyo yalivyo maisha,
Tunapita panda shuka,
pengine hujipitisha,
Penye tabu na kuchoka,
Mara tabu zinaisha,
tunaanza kujicheka,
ndiyo hali ya maisha,
Kila hali tunafika.

Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)