MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
SABABU ZA WANAFASIHI KUCHELEWA KUBAINISHA UTANZU WA NGOMEZI KATIKA FASIHI SIMULIZI

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
SABABU ZA WANAFASIHI KUCHELEWA KUBAINISHA UTANZU WA NGOMEZI KATIKA FASIHI SIMULIZI
#1
Kwa Muhtasari
HISTORIA ya ngomezi ni kongwe kama ilivyo historia ya uumbaji wenyewe. Katika sehemu nyingi za Afrika, ngomezi hutumika kama njia ya mawasiliano, kutoa tahadhari na kuburudisha watu katika makasri ya wafalme na watawala au hata nyakati za sherehe. 
Hata hivyo, kwa upande mwingine, utanzu huu ni mchanga kuliko tanzu zote nyinginezo za fasihi simulizi na si utanzu unaoeleweka vizuri sana miongoni mwa wanafunzi wa Fasihi ya Kiswahili. 
Tunauchukulia kuwa ni mchanga kutokana na ukweli kwamba ni utanzu ambao haujaanza kubainishwa zamani sana japo umekuwapo katika jamii mbalimbali kwa muda mrefu. Labda kutotambulika kwake kulitokana na wanafasihi kusita kuitambua ngoma kama kazi ya fasihi. 
Ngoma kwa uasili wake huonekana kama aina ya sanaa za maonyesho, lakini si fasihi kwa kuwa fasihi ni sanaa ambayo ni lazima itumie lugha kuwasilisha maudhui kwa jamii lengwa. 
Kwa kuwa ngoma katika makabila mengi huwa ni midundo tu isiyokuwa na lugha yoyote itokayo katika midundo hiyo, wanafasihi wengi waliacha kubainisha uwezekano wa kuwa na fasihi ngoma. 
Ukweli ni kuwa upo uwezekano wa kuwa na ngoma ambayo inatoa ishara za lugha (maneno). Ngoma hizo kwa kawaida huwa ni tofauti na ngoma za kawaida na ndiyo maana wanafasihi wengi huziita ngomezi. 
Sababu ya pili iliyosababisha utanzu wa ngoma kuchelewa kubainishwa na wanafasihi ni kuwa aina hii ya fasihi haipatikani katika jamii nyingi sana kama zilivyo tanzu nyingine za fasihi simulizi.
Utanzu huu unasemwa kuenea sana katika jamii za Afrika Magharibi na tafiti za hivi karibuni zimejaribu kubainisha kuwa upo uwezekano wa fasihi hii kuwapo katika jamii za Afrika Mashariki.
Utanzu wa fasihi ngoma au ngomezi umeelezwa sana na wanafasihi katika maandiko mbalimbali. 
Katika utafiti wake kuhusu ngoma, Nketia (1974) katika kitabu chake “The Music of Africa” alibaini kuwa kuna aina tatu za ngoma ambazo ni ngoma za ishara (signal drumming), ngoma za kuchezwa (dance drumming) na ngoma za kifasihi/ngomezi ( talking drums). 
Uainishaji huu unatupa ufahamu kuwa si kila aina ya ngoma ni ngoma za kifasihi (ngomezi). Zipo ngoma ambazo hazina ufasihi wowote.
Ufasihi wa ngomezi unatokana na ukweli kuwa ni ngoma ambazo hugeza vidatu na toni za lugha ya mazungumzo.
Milio ya ngomezi inaweza kurekebishwa kulingana na jinsi wapigaji wanavyozipiga na kubadilisha nguvu wanayoitumia katika kupiga.
Mapigo hayo, kwa hiyo, hugeza sauti ya watu wanaoongea na ndiyo maana huitwa ngomezi. Fasihi ngoma hutoa sauti za kimapokeo zilizozoeleka katika jamii kama vile methali au majigambo na hivyo kueleweka kirahisi miongoni mwa wanajamii.
Neno la Kiingereza la utanzu huu “talking drums” linasawiri uhalisi wa kile ngoma hizi zinachokifanya; ngoma hizi zinaongea.
Hivyo, ngomezi ni tofauti na aina nyingine za ngoma ambazo haziongei bali hutoa midundo tu kwa makusudio maalum kama vile kuburudisha, kutoa taarifa na kadhalika.
Aidha, ngomezi hazikueleweka kwa mtu yeyote bali kwa watu wenye ujuzi na lugha inayogezwa. Vilevile, ngoma hizi zilipigwa na wapigaji maarufu waliobobea katika upigaji wake, si kila mtu aliweza kuzipiga ngoma hizi.
Katika historia ya Afrika, fasihi ngoma imekuwa ikitumika kwa malengo mbalimbali. Malengo hayo, hata hivyo, yamekuwa yakibadilika kulingana na wakati na jamii husika. 
Baadhi ya malengo ya fasihi ngoma katika jamii za jadi za Kiafrika ni pamoja na kutoa taarifa kwa vijiji vya mbali na kuwaleta watu pamoja kama vile kuitisha mikutano.
Aidha, ilisaidia kusuluhisha migogoro miongoni mwa wanajamii na kutunza kumbukumbu muhimu za kihistoria na hivyo kuwakumbusha watu matukio hayo ya kihistoria pindi zinapopigwa.
Mbali na matumizi hayo, fasihi ngoma ilitumika nyakati za sherehe, kama vile za kusimika watawala na machifu, harusi, sherehe za kuwapa watoto majina au mazishi ya watu maarufu.
Ngoma zilipopigwa wakati wa kusimikwa watawala, ngomezi ziliwatahadharisha viongozi hao kutofanya mambo yasiyokubalika miongoni mwa wanajamii.
Katika jamii ya kisasa, fasihi ngoma inatumika kutukuza au kuwakashifu watu wengine, kuwakaribisha wageni, kuisifu miungu na watu katika jamii, kuita mizimu, wahenga na mizuka, kusahihisha makosa ya wanajamii, kutoa mazungumzo ya kimethali ili kuwawezesha watu kuwasiliana na wazee na pia ni sehemu ya sherehe za kifalme au majigambo ya jamii.
Hii inabainisha kuwa malengo na matumizi ya fasihi ngoma, kama ilivyo kwa tanzu nyingine za fasihi simulizi, ni mambo yanayobadilikabadilika kulingana na jamii na wakati. 
Mabadiliko haya ya matumizi ya fasihi ngoma ni ithibati kuwa si kweli kwamba tanzu za fasihi simulizi hurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine, bali hubadilika kulingana na wakati husika.
Kutokana na ukweli huu tunaweza kusema kwamba baadhi ya ngomezi za kisasa ni ving’ora kwenye vyombo vya kusafiria, kengele shuleni, kipenga katika uwanja wa mchezo, mkirizo wa simu, nk.
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)